Wakati Wanawake Duniani wakijiandaa kuadhimisha siku yao kesho Machi 8 inayofanyika kila mwaka Shirika la Marie Stopes Tanzania limesema kwa Mwaka 2022 limeweza kuwafikia wateja zaidi ya Milioni 1.6 kwa kuwapa Huduma na Elimu za Afya ya Uzazi ukilinganisha na Mwaka 2021.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo V.S.Chandrashekar wakati akizungumza na vyombo vya habari leo.

Chandrashekar amesema Shirika hilo limekuwa likitoa elimu ya huduma ya afya ya Uzazi kwa kishirikiana na Serikali na asilimia 95%

ya huduma zitolewazo ni maeneo ya Vijijini hasa kwenye maeneo yasiyofikika kwa urahisi(Hard to reach areas).

"Kuna umuhimu wa kangalia Sera zilizopo kwa kuwa elimu na huduma za Afya ya Uzazi zinasaidia kuondoa au kupunguza changamoto zitokanazo na ukosefu wa elimu na huduma hizo,'amesema ChandraShekar.

Katika kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani tunatoa rai kwa Serikali, mashirika mbalimbali na watu binafsi kuwekeza zaidi katika huduma ya Afya ya uzazi kwa kuwa ubora wa Afya ndio msingi wa kuwa na taifa bora
Mkurugenzi mkazi wa  Shirika la Marie Stopes Tanzania V.S Chandrashekar akizungumza na waandishi wa habari
Dkt. Geoffrey Sigalla (kushoto) na Mkurugenzi mkazi wa  Shirika la Marie Stopes Tanzania V.S Chandrashekar  ​wakiwa katika picha ya pamoja wakati wakizungumza na vyombo vya habari leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...