Afisa
Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti Breweries, Emila Tom Machuve
(kulia) akizungumza na mmoja wa washindi wa promosheni ya bia ya Pilsner
ijulikanayo kama ‘Kapu la Wana’ wakati wa droo ya tatu ya promosheni
hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mwakilishi kutoka
bodi ya michezo ya kubahatisha ya Tanzania, Salim Mgufi akisimamia
mchakato huo. Kwenye droo hiyo, walipatikana washindi saba kutoka kanda
ya Ziwa, Kusini na Kaskazini ambapo promosheni ya Kapu la Wana
inafanyika.
Kati ya washindi hao, watatu walijishindia simu
janja, wengine watatu walijishindia televisheni za kisasa na mmoja
alijishindia pikipiki. Washindi hao wanatarajiwa kukabidhiwa zawadi zao
tarehe 18 mwezi huu. Promosheni ya Kapu la Wana ilizinduliwa tarehe 02
mwezi wa pili. Droo inayofuata itakuwa ya mwisho ambapo zawadi kubwa ya
gari itapatikana.
Mwakilishi
kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha ya Tanzania Salim Mgufi (kushoto)
akizungumza jambo wakati wa droo hiyo iliyofanyika jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Afisa Masoko wa Serengeti Breweries, Emila Tom Machuve.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...