Na.VERO IGNATUS,MWANZA.

Katika kipindi cha miaka mitatu 2020 hadi 2022 ajali za barabarani , zimeua watu 4060 na kujeruhi watu 6427,kufuatia hali hiyo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa maagizo 11,yatakayosaidia kudhibiti tatizo hili hivyo alizitaka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Jeshi la Polisi na Baraza Taifa la usalama Barabarani kuhakiksha wanatekeleza mambo hayo

Akizungumza katika ufunguzi wa Maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama, ambayo Kitaifa yalifanyika mkoani Mwanza,aisema kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzi 2020 eneo linalongoza kwa ajali ni sekta ya usafirishaji wa abiri na kusababi vifo 1582 vya abiria na 4372 walipata majeraha na ulemavu,watembea kwa miguu 959 walipitiwa na vyombo vya moto.

Ajali za barabarani zimekuwa ni chanzo cha maumivu na majonzi kwa jamii,kupoteza wa wapendwa wetu,mali,vyombo vya moto na ulemavu wa kudumu kwa ndugu zetu,zinaua na kupoteza nguvu kazi nyingi ikiwemo wafanyakazi katika sekta ya umma na binafsi wakti mwingine ata wanafunzi wa taaluma ya makundi mbalimbali,”ameeleza Majaliwa.

Majaliwa amesema Baraza la Taifa la usalama barabarani likamilishe kwa haraka maboresho ya sheria ya Barabani Ili kukabiliana matumizi mabovu ya barabara na njia,ikiwa ni kuhakikisha alama za barabarani zinakuwepo katika maeneo hatarishi,ili kuwabaini maderevya wanaokaidi sheria na kusababisha ajali 5132 kwa kipindi cha mwaka 2020 hadi 2022 ambazo ziliripotiwa katika vyombo vya usalama.

"Katika kuhakikisha ajali za barabarani zinapungua,Baraza la Usalama Barabani Taifa linashirikiana na wadau mbalimbali katika kukabiliana na adha mbalimbali zinazojitokeza kwa wananchi zinazohusiana na ajali,huku tukitoa tafadhari Kwa jamii kuacha kushabikia vitendo vya ukiukwaji wa sheria hususani kumchochea dereva kwenda mwendo kasi,"alisema Ng'anzi..

Kwa upande wa watembea kwa miguu Majaliwa ameeleza kuwa kwa kipindi hicho cha miaka mitatu watembea kwa miguu 959 walipitiwa na vyombo vya usafiri walipokuwa wanatembea barabarani huku 650 walijeruhiwa kutokana na ajali za barabarani wakitembea kwa miguu.

“Idadi hii nayo haipendezi kuitamka ni kubwa tunapotumia vyombo vya moto barabarani lazima tuhakikishe tunazingatia watembea kwa miguu,na wale wanaotembea kwa miguu kando kando ya barabara lazima wazingatie matumizi sahihi ya barabara,”ameeleza Waziri Mkuu.

" Ajali za waendesha pikipiki kundi hilo siyo tu waendesha bodaboda hao kwa ajili ya biashara hata wale wanaofanya kwa matumizi binafsi kwa kipindi cha miaka hiyo mitatu wapanda pikipiki 797 walifariki huku 725,walijeruhiwa, Kundi jingine ni wapanda baiskeli ambao kwa kipindi hicho 196 walipoteza maisha na wengine 82,walijeruhiwa idadi hiyo nayo siyo nzuri pia.Alisema Majaliwa

Aidha Majaliwa ameeleza kuwa kwa upande wa wanaoendesha vyombo vya moto katika kipindi hicho madereva 509 wamepoteza maisha huku 584 wakipata majeruhi mbalimbali katika miili yao wakiwa wanaendesha magari huku kundi jingine ni la wavuta na watembeza mikokoteni 17 walipoteza maisha na 14 walipata madhara miilini mwao

Amesisitiza Baraza lihakikishe linakamilisha maagizo ya Dkt Samia Suluhu Hasani la kukagua magari,ili safari zianze kwa watumiaji,huku akiliagiza jeshi la Polisi kukamilisha mifumo ya Kielektoniki itakayo saidia kulinda mwendo wa maderevya ambao hawajali sheria wanaendesha wakiwa wamekunywa pombe,Matumizi ya simu.

Aidha alilitaka Jeshi la Polisi pamoja na kazi nzuri linazozifanya,waendelee kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara,huku akiiagiza wizara ya Elimu,Sayansi na Tekinolojia kuanzisha masomo ya usalama barabarani,kuanzia shule za Msingi, Sekondari hadi Vyuoni,hii itasaidia kuwaandaa Vijana wakiwa bado wadogo katika misingi ya usalama.

"Idadi hii inatisha sana na kwa Tanzania haikubaliki ,upande wapanda pikipiki za biashara na binafsi watu 797 walifariki na 725 walijeruhiwa, wandesha baiskel 196 walipoteza maisha, majeruhi 584 na wajasilia mali ambao ni wasukuma mkokoteni 17,majeruhi 14,hivyo jitihada za pamoja zinahitajika ili kupunguza au kuondoa ajali za barabarani ambazo zimekuwa ni tishio kwa maisha ya watanzania,"alisema Majaliwa.

Aidha Majaliwa alisema mabasi yanayonda safari ndefu za mikoani ni miongoni mwa wahanga wa ajali za barabarani,kutokana na kutokufuata kanuni za kutokuwepo na maderevya wa akiba katika gari hizo,huku akizitaka Kampuni zinazotoa huduma za safari ndefu kuweka maderevya zaidi ya mmoja watakaosaidiana kuendesha,ili kuepuka ajali zitokanazo na derevya kuchoka.

Akitoa salamu za Jeshi la Polisi,Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Kamilius Wambura amesema, kumekuwepo na tabia ya mifumo mibovu ya upatikanaji wa maderevs kutokana na Vyuo kushindwa kufuata weledi na kutoa vyeti vya kugushi kwa maderevya ambao wengi wamekuwa ni chanzo cha ajali.

""Tumeanzisha oparesheni kwa madereva Ili kubaini waliopata leseni kinyume na utaratibu,tunaendelea kutambua elimu ndiyo nyenzo ya kujikinga na ajali za barabarani Jeshi la Polisi linazingatia umuhimu huo,tunaishukuru Serikali kwa ufumbuzi wa kelo ya wananchi waliokuwa wakidai chanzo cha ajali ni ubovu wa miundombinu,kwa sasa barabara zote zinapitika vizuri

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima amewataka wananchi walio kandokando ya barabara kutojichukulia sheriamkononi inapotokea ajali katika maeneo yao,kujiepusha kuchoma matairi,kuweka magogo kwania ya kufunga barabara,hivyo kuleta usumbufu kwa watumiaji wa barabara ambao wanamatatizo mbalimbali.

"Tunashukuru Mkoa wetu wa Mwanza,umekuwa kinara wa kuheshimu masuala ya usalama barabarani,maana tunazingatia kutoa elimu ya usalama barabarani,kutokana na kutambua chanzo cha ajali ni makosa ya kibinadamu yanayoweza kuzuilika tunaendel kuwapatia elimu wananchi juu ya kushirikiana kwa pamoja ajali zitapungua ,"alisema Malima.

Aidha Katibu mtendaji wa Baraza la Taifa la usalama Barabani Kamishina Mwandamizi msaidizi wa Jeshi la Polisi Ramadan Ng'anzi alisema,baraza linaendelea kuwakumbusha madhara ya tokanayo na ajali za barabarani Kwa madereva,bodabida, Walimu Kwa kuwapa mafunzo ya usalama barabarani


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...