Njombe
Malori kadhaa yaliyokuwa yakitoka vijijini kubeba mizigo mbali mbali ikiwemo viazi katika maeneo ya Luponde halmashauri ya mji wa Njombe yametekwa na watu ambao bado hawajafahamika March 18 majira ya saa nne usiku na kuwachapa viboko madereva ili kuwashinikiza kutoa fedha.
Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issah ametoa ufafanuzi juu ya tukio hilo mara baada ya kuzungumza na kutoa elimu mbali mbali kwa madalali pamoja na madereva katika kituo cha malori ya mizigo kilichopo eneo la Edina mjini Njombe.
"Jana usiku gari zimekuta magogo yamewekwa na haya ni miti iliyokatwa kwa ajili ya kutengeneza barabara kwa hiyo wakati huo dereva akitoka kwa ajili ya kuangalia gogo ndio walikuwa wanamkamata wanampekua,wanamtandika viboko na wakati zoezi hilo linafanyika magari yalikuwa mengi,baadaye lilikuja gari la maji na ninaona walikuwa wanaisubiri kwa kuwa ilitoka kwenye mauzo ya maji na kuchukuliwa kiasi cha laki nane ambapo ukijumlisha na wengine inafika milioni moja na nusu"alisema Kamnda Issah
Aidha kamanda Issah amesema hakuna madhara yeyote yaliyotokea kwa binadamu wala magari na tayari yameendelea na safari huku akiahidi kupanga mikakati zaidi na madereva pamoja na madalali ili kuhakikisha wanakuwa salama wanaposafirisha mizigo yao.
Tukio hili linajiri ikiwa ni takribani wiki tatu zimepita tangu ulipotokea utekaji wa malori ya mizigo yaliyokuwa yakitoka mnadani pamoja na basi la abiria katika eneo la kati ya Nyombo na Kidegembye huko Lupembe wilayani Njombe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...