Na Jane Edward, Arusha

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Dkt Suleimani Jafo amevitaka viwanda vyote Nchini kuiga mfano wa kiwanda cha Lodhia kilichopo jijini Arusha kwa kutunza na kuhifadhi mazingira.

Jafo ameyasema hayo alipokuwa katika ziara yake ya kikazi ya ukaguzi wa kiwanda hicho cha nondo pamoja na kulenga kuanzisha mpango wa kutengeneza kiwanda cha mabati ili kutoa ajira kwa vijana wa kitanzania.

“Lodhia ni kiwanda cha mfano wa kuigwa kwani ni kiwanda ambacho kinalinda mazingira yanayozunguka kiwanda hicho kwa manufaa ya afya za watanzania"Alisema Jafo

Naye Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda hicho Sulesh Pandit alisema wanashukuru kwa ujio wa Waziri katika kiwanda hicho na kwamba wako tayari kushirikiana na wizara ya mazingira katika masuala mbalimbali ili kuboresha mazingira hapa nchini.

Katika ziara hiyo Waziri Jafo pia alitembelea kiwanda cha Bansal cha jijini Arusha kinacho tengeneza Nondo ambapo alisema kiwanda hicho kina changamoto ya kimazingira na kuwataka kufuata kanuni za mazingira ili kuwa salama.

"tunatambua michango ya wawekezaji wadogo lakini suala la uboreshaji mazingira ni muhimu ili kuweka mazingira salama pamoja na afya za wananchi"

alipanda mti katika kitalu cha miti cha Kiwanda hiko kama ishara ya kuonesha umuhimu wa upandaji miti na kusisitiza jamii kuhifadhi na kutunza mazingira kwa kupanda miti kila siku.

“Niwapongeze sana kwa juhudi zenu katika utunzaji wa mazingira kwa kuanzisha kitalu hiki cha miti ambapo kwa sasa tuko kwenye kampeni muhimu ya kupanda miti mmeonyesha kitu kikubwa sana”.

Naye meneja wa baraza la uhifadhi na usimamizi wa mazingira NEMC kanda ya kaskazini Lewis Nzali alimuahidi Waziri Jafo kusimamia kiwanda hicho ili waweze kukamilisha taratibu za kimazingira.

"Sisi kama wasimamizi wako wa mazingira tuna kuahidi kusimamia mazingira sio kwa kiwanda hiki tu hata vingine ambavyo havijafata taratibu za kimazingira zinazotakiwa"Alisema Nzali.
Mkurugenzi akiwapa maelezo kuhusu kiwanda hicho.
Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha LODHIA Sulesh Pandit akisalimiana na Waziri Jafo mara baada ya kuwasili kiwandani hapo.
Waziri Jafo akitoa maelekezo alipofika kwenye kiwanda cha Bansal jijini Arusha.
Vijana wa kiwanda cha LODHIA wakipanga Nondo mara baada ya kukamilika kwa utengenezaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...