Na Pamela Mollel,Arusha

Bondia anayetamba hivi sasa katika Jamuhuri ya demokrasia ya Kongo
Madrose Katembo Kuvesa amewasili nchini Tanzania nakupata fursa ya kutembelea Vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo hapa nchini

Mara baada ya kuwasili katika hifadhi ya Taifa Tarangire Mkoani Arusha akitokea katika michoro ya Miamba ya Kolo wilayani Kondoa Mkoani Dodoma Bondia Kuvesa amekiri kuridhishwa na vivutio vilivyopo katika za taifa la Tanzania.

Amesema kuwa fursa aliyopata ya kutembelea vivutio hivyo itamuwezesha kuitanga Tanzania katika soko la utalii ambapo atahamasisha wageni mbalimbali kufika na kujionea vivutio vinavyopatikana Tanzania

Kabla ya kufanya utalii huo alifanya pambano la kirafiki dhidi ya Bondia mwenzake raia wa Tanzania Hassan Mwakinyo lenye kuhamasisha uchangiaji wa Taulo za kike na kupatiwa fursa ya kuwa balozi wa kutangaza vivutio vya utalii vya Taifa ambapo mara baada ya kutembelea hifadhi hii ya Taifa Tarangire bondia kuvesa anawapa taarifa ya Fursa kwa wawekezaji kuwekeza nchini Tanzania kwani ndio mahala pekee duniani penye mazingira ya asili na wanyama wote wakubwa

Akizungumzia manufaa ya ujio wao kwa shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA) Afisa uhifadhi daraja la II hifadhi ya Taifa Tarangire Hilda Mikongoti amesema bado wanaendelea kuutangaza utalii kwa njia mbalimbali huku akieleza kuwa wapo tayari kupokea kila aina ya ugeni kutoka ndani na nje ya Tanzania.

"Uwepo wa mabondia hawa utawezesha kutangaza utalii wetu ndani na nje ya nchi,hivyo sisi kama wahifadhi tumejipanga vyema kupokea wageni mbalimbali "alisema Mikongot






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...