Na Mwandishi Wetu,Same

MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali wa Wilaya hiyo Kwa kuhakikisha wananufaika na shughuli za kilimo kikiwemo cha tangawizi.

Mgeni ametoa kauli hiyo alipotembelea kiwanda cha kuchakata Tangawizi kilichopo kata ya Myamba katika Jimbo la Same Mashariki ambacho kwa kiasi kikubwa hutegemewa na wakazi wa maeneo hayo ambao wengi wao wanaojishugulisha na kilimo cha tangawizi na kiwanda hicho kimekuwa na manufaa makubwa kwao.

"Tunamshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassani kwa kuwajali wakulima kwani pamoja na mambo mengine awezesha kiwanda hiki kuendelea kuchakata tangawizi na kuipandisha thamani na sote tunafahamu kiwanda hiki ni matokeo ya uwezekeza wa ubia baina ya ushirika wa wakulima wa tangawizi na Mfuko wa PSSSF,"amesema.

Amewasisitizia viongozi wa kiwanda hicho kuhakikisha wanaendelea na uzalishaji kuwawezesha wakulima kuwa na soko la uhakika huku akiwataka wakulima nao kuchangamkia fursa ya uwepo wa soko la tangawizi ili kukuza kipato.
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...