KATIBU Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, amesema nia kuu ya Wizara hiyo kwa sasa ni kufanya uhifadhi na kutangaza utalii kwa viwango vya kimataifa.

Dkt. Abbasi ameyasema hayo leo Aprili Mosi, 2023 alipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi na kukutana na viongozi wa hifadhi hiyo iliyopo Morogoro ambapo pia aliendesha kikao cha Kamati ya Utekelezaji ya Mradi wa Kuendeleza Utalii wa Maeneo ya Kusini mwa Tanzania (Regrow).

“Tutahifadhi na baada ya kuhifadhi tutatangaza na maono ya viongozi wetu kwa sasa kupitia kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Waziri wetu Mhe. Mohamed Mchengerwa ni kujipanga kuutangaza utalii wa Tanzania Kimataifa zaidi, niwaahidi tu kwamba hatutakiwa na jambo dogo,” alisema Dkt. Abbasi.
Ameongeza kuwa hizi ni zama za Royal Tour, akisisitiza kuwa kama Rais Samia alitoka na kuutangaza utalii wetu kwanini sisi tujifungie maofisini na kuwahimiza viongozi hao kutumia teknolojia za kisasa kuhifadhi na kutangaza utalii wetu.

“Kuna mtafiti mmoja pia ameonesha watu wengi nchini hawaendi kutalii kwasababu wana woga wa gharama na namna ya kufika kwenye maeneo husika.

“Tuanzishe vifurishi mbalimbali vya kuwavuta watalii wa ndani na nje, sikukuu zinakuja je tumejipanga vipi kutangaza vivutio vyetu, je watu wanajua bei zetu na kwanini tusiwe na vifurushi maalum kwa ajili ya hizi sikukuu, naamini tunaweza kupata watalii wengi kupitia hizi sikukuu,” alisisitiza.
Akiongoza Kikao cha ziada cha Kamati ya Uongozi ya Mradi wa REGROW, Dkt. Abbasi amesema mradi huo umechelewa kwa sababu mbalimbali na kuagiza kuwa kila taasisi husika ihakikishe kwa siku zilizobaki za mradi hakuna mkandarasi anaongezewa muda bila hoja zito na wasioweza waondolewe mapema kabla hata ya kusaini mikataba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...