Na Farida Ramadhani, WFM – Dodoma
Serikali
imesema inaendelea kutekeleza sheria katika ufuatiliaji na tathmini ya
misamaha ya kodi ikiwemo Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ili
kuhakikisha kuwa misamaha ya kodi inatolewa kwa kuzingatia sheria na
inatumika kama ilivyokusudiwa.
Hayo yameelezwa bungeni jijini
Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande
(Mb) alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kibamba, Mhe. Issa Jumanne
Mtemvu aliyetaka kujua mkakati wa Serikali kuhakikisha Misamaha ya VAT
inayotolewa inaleta tija kama ilivyokusudiwa.
Mhe. Chande
alisema ili kuhakikisha misamaha ya kodi inakuwa na tija katika uchumi
na jamii kwa ujumla, orodha ya bidhaa na vifaa vinavyostahili msamaha wa
kodi inaandaliwa na kuhakiki orodha ya bidhaa na vifaa.
“Tunahakikisha
mwombaji anajaza fomu maalum inayothibitisha ununuzi wa bidhaa au vifaa
husika pamoja na kufanya kaguzi za mara kwa mara dhidi ya misamaha
iliyotolewa ili kuthibitisha iwapo matumizi ya bidhaa au vifaa
vilivyosamehewa kodi vimetumika kama ilivyokusudiwa”, aliongeza Mhe.
Chande.
Alisema pia Wizara ya Fedha na Mipango kwa kushirikiana
na Mamlaka ya Mapato Tanzania inaendelea kutekeleza matakwa ya kisheria
katika ufuatiliaji na tathmini ya misamaha ya kodi ikiwemo Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) ili kuhakikisha kuwa misamaha ya kodi
inatolewa kwa kuzingatia sheria na inatumika kama ilivyokusudiwa.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) alipokuwa akijibu swali, bungeni jijini Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...