BODI ya Utalii Tanzania (TTB) inashiriki katika onesho la Nne la Takulandirani Malawi International Tourism Expo kwa lengo la kutekeleza mkakati wa ushirikiano wa kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC

Onesho hili la Utalii linahudhuriwa na washiriki kutoka nchi mbalimbali duniani, linafanyika katika ukumbi wa Bingu wa Mutharika International Conference Centre (BICC) mjini Lilongwe kuanzia leo tarehe 26 mpaka 27 Aprili, 2023.

Banda la Tanzania limekuwa na mwitikio mkubwa wa kutembelewa wageni wenye shauku ya kutaka kupata maelezo kuhusu vivutio vya utalii vya Tanzania hasa Hifadhi ya Serengeti , Mlima Kilimanjaro na visiwa vya Zanzibar ambavyo ni baadhi ya maeneo katika filamu ya The Tanzania, Royal Tour iliyoasisiwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Hayo ameyasema na Afisa Utalii wa TTB, Alistidia Karaze ambaye anaiwakilisha Bodi katika ushiriki wa onesho hili. Ameongeza kuwa ushiriki wa maonyesho haya unatoa fursa ya kuuza vivutio vya nchi wanachama wa SADC kwa Pamoja, ambapo mtalii anaweza kutayarishiwa safari ya kutembelea vivutio vya nchi mbili au zaidi kama kifurushi kimoja (Single Package).

Onesho hili linaloandaliwa na Wizara ya Utalii ya Malawi linatarajiwa kufanyika kila mwaka nchini Malawi.
Afisa Mawasiliamo wa Shirika la Utalii Duniani, Kojo Kuntum akionesha taarifa aliyoiandika kuhusu Bodi ya Utalii Tanzania wakati alipotemblea Banda la Tanzania.
Waziri wa Utalii wa Malawi, Mheshimiwa Vera Kantukule akisilikiza maelezo kutoka kwa Afisa Utalii wa Bodi ya Utalii alipotembelea Banda la Tanzania


Baadhi ya Wageni wakiwa katika banda la Tanzania wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Utalii wa TTB, Alistidia Karaze wakati wa Onesho la Utalii linalifanyika nchini Malawi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...