Wanafunzi 20 wamehitimu Kozi ya Mafunzo ya Kurusha Ndege Zisizo na Rubani katika Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) ikiwa ni sehemu ya Mradi wa Kuimarisha Huduma za Afya ya Mimea nchini Tanzania kwa ajili ya kuhakikisha Usalama wa Chakula.

Mahafali hayo yamefanyika katika viwanja vya Makao Makuu ya TCAA Banana - Ukonga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa ushirikiano wa kimaendeleo wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Cedric Merel ambao ndio wadhamini wakuu wa mradi huu utakaotekelezwa kwa miaka mitatu unaolenga kutatua mapungufu ya kiuendeshaji na ya kiufundi yanayohusiana na afya ya mimea ambayo yanazorotesha biashara ya kilimo na kuhatarisha usalama wa chakula nchini Tanzania.

Wengine waliohudhuria Mahafali hayo ni na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (FAO) Dkt. Nyabengi Tipo, Mkurugenzi Idara ya Kilimo na Usalama wa Chakula -SMZ Hamad Masoud, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Daniel Malanaga, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Udhibiti wa Viuatilifu Tanzania (TPHPA) Prof. Joseph Ndunguru na Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga (CATAC).

Mradhi huu umeratibiwa na Umoja wa Ulaya(EU) kwa kushirikiana na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) pamoja na Wizara ya Kilimo Nchini kupitia Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA).
Mkuu wa ushirikiano wa kimaendeleo wa umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Cedric Merel akizungumza kuhusu Ushirikiano kati ya Tanzania na Umoja wa ulaya katika kusimamia na kuendeleza kilimo hapa nchini kwa kutoa misaada mbalimbali mahafali ya 10 kwa wahitimu wa mafunzo ya Ndege nyuki ‘Drone’ yanayotolewa na Chuo cha Usafiri wa Anga(CATC) yaliyosimamiwa na Umoja wa Ulaya(EU) kwa kushirikiana na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) pamoja na Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA).
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (FAO) Dkt. Nyabengi Tipo akizungumza namna Shirika hilo lilivyoweza kusimamia mradi wakati wa mahafali ya 10 kwa wahitimu wa mafunzo ya Ndege nyuki ‘Drone’ yanayotolewa na Chuo cha Usafiri wa Anga(CATC) yaliyosimamiwa na Umoja wa Ulaya(EU) kwa kushirikiana na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) pamoja na Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA).
Mkurugenzi Idara ya Kilimo na Usalama wa Chakula -SMZ Hamad Masoud akizungumza namna Serikali ya Zanzibar ilivyojipanga kuendeleza kilimo japo kuna changamoto ya Aridhi wakati wa hafla ya kuwatunuku vyeti wahitimu wa Mafunzo ya Ndege nyuki ‘Drone’ yanayotolewa na Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) kwa kutumia wataalam wa ndani.
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga(CATC) kinachomilikiwa na TCAA, Aristide Kanje akizungumza kuhusu namna walivyoweza kutoa mafunzo kwa kutumia wataalam wa ndani waliofanikisha watahiniwa wa mafunzo ya Ndege nyuki ‘Drone’ yanayotolewa na chuo hicho wakati wa mahafali ya 10 yaliyofanyika katika viwanja vya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania ( TCAA) jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Udhibiti wa Viuatilifu Tanzania (TPHPA) Prof. Joseph Ndunguru akizungumza namna Mamlaka hiyo ilivyoweza kusimamia mradi kuimarisha Huduma za Afya ya Mimea nchini Tanzania wakati wa mahafali ya 10 kwa wahitimu wa mafunzo ya Ndege nyuki ‘Drone’ yanayotolewa na Chuo cha Usafiri wa Anga(CATC) yaliyosimamiwa na Umoja wa Ulaya(EU) kwa kushirikiana na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) pamoja na Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA).
Mkuu wa ushirikiano wa kimaendeleo wa umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Cedric Merel akiwatunuku wahitimu wa mafunzo ya urubani wa Ndege nyuki (Drone) wakati wa mahafali ya 10 yaliyofanyika katika viwanja vya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania ( TCAA) jijini Dar es Salaam.
Mhitimu Masoud Matimbwa akitoa neno la Shukrani kwa wafadhili wa Mradi wa Kuimarisha Huduma za Afya ya Mimea nchini Tanzania uliokuwa unaratibiwa na Umoja wa Ulaya(EU) kwa kushirikiana na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) pamoja na Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA).
Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Daniel Malanga akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Hamza Johari wakati wa hafla ya kuwatunuku vyeti wahitimu wa Mafunzo ya Ndege nyuki ‘Drone’ yanayotolewa na Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) kwa kutumia wataalam wa ndani.
Mkuu wa ushirikiano wa kimaendeleo wa umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Cedric Merel, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Udhibiti wa Viuatilifu Tanzania (TPHPA) Prof. Joseph Ndunguru, Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Daniel Malanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na wahitimu wa mafunzo ya urubani wa Ndege nyuki (Drone) wakati wa mahafali ya 10 yaliyofanyika katika viwanja vya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania ( TCAA) jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...