Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha ACT-Wazalendo kimetoa mwito kwa jamii kuhakikisha watoto wanalindwa ili kufikia malengo yao sambamba kuwa viongozi imara kwa maslahi ya taifa.
Taarifa iliyotolewa leo Mei 4,2023 na Chama hicho imeeleza kwamba hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Tanzania Bara Dorothy Semu alipokuwa katika kituo cha kulea watoto yatima cha Sara House kilichopo Mwandege wilayani Mkurunga mkoa wa Pwani.
Dorothy ametembelea kituo hicho akiwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa wa Chama ama hicho pamoja na Janeth Rithe Naibu Katibu wa Uenezi , Bonifacia Mapunda Katibu wa Ngome ya wanawake, Sevilina Mwijage Mjumbe wa Halmashauri Kuu, na Mwenyeji wao Mohammed Mtambo Katibu wa ACT-Pwani,na wanachama wengine waandamizi wa Chama hicho.
Dorothy amesema kuwa ni muhimu kuwalinda watoto ni pamoja na kuhakikisha kuwa wanakuwa salama kisaikolojia na kimwili ili kupata viongozi imara watakaoliongoza taifa .
"Suala la ulinzi wa watoto ni wajibu wetu sote ,kila mtu ahusike katika kumlinda mtoto wa Kitanzania ili kuhakikisha watoto wetu wanakuwa salama na kuepushwa madhara yakisaikolojia ,au kimwili ", Dorothy.
Amesema kuwa ripoti za haki za Binadamu ha mwaka 2022, ilionyesha kuwa matendo ya unyayasaji watoto yameongezeka na kwamba hali hiyo haina ustawi mzuri wa watoto.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...