Benki ya Exim Tanzania imeboresha mfumo wake mkuu wa huduma za kibenki ikilenga kutoa huduma bora kwa wateja wake.

Kwa mujibu wa taarifa ya benki hiyo iliyotolewa mapema jana ilitaja kuwa mfumo huo mpya unarahisisha uchakataji wa miamala, hatua za usalama zilizoboreshwa, na utendaji kazi ulioimarishwa, ambao utahakikisha matumizi salama na rahisi zaidi ya benki kwa wateja.

Kupitia taarifa hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Bw. Jaffari Matundu alisema kuwa mfumo huo mpya umeundwa ili kutoa suluhisho la huduma za kibenki kwa wateja hao na kuwawezesha kufanya miamala yao ya kifedha kwa urahisi na utulivu wa akili.

Aidha Bw Matundu alitoa shukurani zake kwa wateja wa benki hiyo kwa ushirikiano na uvumilivu wao wakati wa uboreshaji huo huku akiomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kutokana na changamoto za mpito zinazojitokeza katika baadhi ya huduma kufuatia maboresho hayo.

Naye Afisa Mkuu wa Teknolojia wa benki hiyo na Mkuu wa Kitengo cha Mabadiliko ya Kidijitali, Bw. Alamin Merchant, alisema mfumo huo ulioboreshwa unatoa huduma na manufaa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na huduma za ziada za benki mtandaoni, taarifa (notifications) kwa wakati halisi, na programu ya huduma za benki kupitia simu ambayo ni rafiki na inayomfaa mtumiaji.

Bw. Merchant alionyesha shauku yake katika kuwapatia wateja suluhisho sahihi na huduma zilizoboreshwa hususani katika ufanyaji wa miamala, utendakazi ulioimarishwa, na hatua za usalama zilizoboreshwa.

Alisisitiza kuwa mfumo huo mpya umeundwa ili kufanya huduma za benki kufikiwa kwa urahisi zaidi na wateja sambamba na kuhakikisha kwamba akaunti zao na taarifa zao binafsi ziko salama kila wakati. Benki imejitolea kuendelea kuboresha huduma zake ili kukidhi mahitaji yanayoendelea ya wateja wake.

Katika kuhitimisha taarifa hiyo Bw. Matundu alitoa shukrani zake kwa wateja kwa kuchagua Benki ya Exim kama mshirika wao wa kibenki na fahari yao katika teknolojia ya kisasa ya kibenki inayokidhi mahitaji yao yanayoendelea.

Aliahidi kuwa benki hiyo inaendelea kutoa uzoefu bora zaidi wa kibenki kwa wateja wake, na uboreshaji huo ni hatua muhimu ya kufikia lengo hilo.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Bw. Jaffari Matundu (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)  katika moja ya matukio ya benki hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...