Na.Vero Ignatus,Arusha.

Waandishi wa habari wametakiwa kuzingatia maadili na sheria za nchi pale wanapotekeleza majukumu yao kwani wanalo jukumu la kuhabatisha jamii mambo mbalimbali yanayoendea katika Taifa na Kimataifa.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. James Ole Millya kwamba bila waandishi wa habari jamii haiwezi kuhabarika, hivyo kuwataka kuwa wakweli na kufunua mambo sambamba na kuepuka masuala ya Udini na Ukabila ambayo yanaweza kuleta changamoto.

Aidha amewataka waajiri kuwalipa waandishi stahiki zao sambamba na kuwapatia mikataba ya kazi pamoja na bima za Afya kwani nao wanafamilia zinazowategemea, huku akiwataka kutokukaa kimya pale wanapodhulumiwa stahiki zao.

"Msijidharau, Jitambueni, kuweni na umoja katika kuhakikisha mnapata stahiki zenu,kwani kazi yenu ni kubwa katika kuhabarisha jamii na Taifa kwa ujumla"alisema Millya

Naye Mwenyekiti wa mwenyekiti wa chama Cha wafanyakazi katika vyombo vya habari JOWUTA,Musa Juma aliwataka wanahabari kutokona aibu kudai haki zao kwani haiwezekani kuwa kibarua, na hawana mikataba kwa miaka 10.

Kwa upande wake muwakilishi wa Shekhe Mkuu wa mkoa Arusha, Shekhe Hamis Kassim yeye alijikita zaidi kusisitiza juu ya maadili pamoja na kuwaasa waaandishi kuhakikisha wanatumia kalamu zao vyema katika kuhakikisha kuwa wanatoa taarifa zilizo sahihi ambazo hazitaleta madhara kwa jamii

Aidha alisisitiza juu ya suala la malezi kwa watoto na kusema kuwa kutokana na mmomonyoko wa NMmaadili uliopo kwa sasa amewataka waandishi kuwa mfano bora wa kuandika habari zinazokemea ukengemfu wa maadili, kwa kukemea mazingira yeyote yale yanayomuelekeza mtoto kupenda tabia ambazo siyo sahihi kama vile za ushoga, kwani jambo hilo linaumiza na halikubaliki.

"Tuwalinde watoto wa kike na wakiume ili wasiiingie katika tatizo hilo ambalo ni chukizo kwa Mungu na kwa jamii, kila mmoja anao wajibu wa kuhakikisha watoto wetu wanakuwa salama."alisema 

Amesema kuwa mtoto kuanzia 0-8 ni kama upepo ambao unategemea na mazingira na jamii inayomzuka kwamba anajifunza nini kutoka kwao.

"Upepo unapovuma kama kuna kuna pilau inapikwa basi utanusa harufu nzuri ya hicho chakula, halikadhalika upepo ulivuma sehemu yeye harufu mbaya vilevile utanusa harufu mbaya ya kukera, mfano huu nauelekeza kwenye malezi na. Makuzi ya mtoto akilelewa vyema kutakuwa na harufu nzuri maishaniwake ila akilelewa vibaya kutokana na mazingira hayo lazima kutakuwa na harufu mbaya mno maishaniwake pia " alisema Shakhe Hamis" 

Aidha maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari yamebeba kauli mbiu isemayo ''Kuunda mustakadhi wa haki uhuru wa kujieleza kama kichocheo cha haki nyingine zote za binadamu.'' 

 

Mbunge wa Bunge la Afrika ya Mashariki James Ole Millya akizungumza na waandishi wa habari katika Kongamano la maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari 20 may 2023 mkoa wa Arusha katika ukumbi wa EAC.   
Waandishi wakimsikiliza mgeni rasmi  Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki James Millya (hayupo pichani) katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari leo mei 20 Jijini Arusha. 
Mwenyekiti wa Arusha Press club APC Cloud Gwandu akizungumza katika Kongamano la maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari 20 may 2023 mkoa wa Arusha katika ukumbi wa EAC. 
 





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...