Na Jane Edward, Arusha
Chuo cha bandari kimesema kimejipanga katika kuhakikisha wanaandaa mitaala katika kutumia fursa ya upatikanaji wa mafuta na gesi .
Hayo yamesemwa na Dr Lufunyo Hussein ambaye ni Mkuu wa chuo cha bandari wakati wa kuzungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya mafunzo ya ufundi stadi yanayoendelea katika uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Dkt Lufunyo Amesema kuwa kwa sasa wanaandaa mitaala katika mafuta na gesi ili kuweza kuzalisha wataalamu watakaokuwa wamebobea kwa kushirikiana na wataalamu wa mradi wa mafuta na gesi.
Amebainisha kuwa chuo hicho cha Bandari kimekuwa kikitekeleza miradi mikubwa kama ya SGR ambapo wataalamu wanaotandika Reli hapa nchini ni zao la chuo hicho.
"Chuo hiki cha bandari ni moja kati ya vyuo ambavyo vinatoa elimu ya ufundishaji wa masuala ya bandari kwa kutoa kozi za muda mfupi na muda mrefu"Alisema Dr Hussein
Amesema kwa sasa wanafanya mashirikiano na nchi zingine katika kuendeleza bandari kwa kuwa wenzetu wa nje ya nchi Wana ustadi mkubwa katika masuala ya bandari.
Akizungumzia uwiano wa wanafunzi wakike katika chuo hicho amesema idadi ya wanaume ni kubwa kuliko wakiume kutokana na hapo awali kulionekana ubebaji wa mizigo ulikuwa ukitumia nguvu.
Aidha amesema kwa sasa wanawakaribisha wanafunzi wakike katika kuendesha zana nzito pamoja na kazi zingine za bandari kutokana na sasa shughuli nyingi hufanywa kwa kutumia mitambo.
Mkuu wa chuo cha Bandari Dr Lufunyo Hussein akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.



.jpeg)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...