Na Mwandishi Wetu Tanga

MKUU wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa amewataka wafanyabiashara na wawekezaji kutumia bandari ya Tanga ambayo imefanyiwa maboresho makubwa ikiwemo kuongeza kina cha maji kutoka mita 3 hadi 13.

Pia upanuzi wa magati yote mawili ambayoyameongeza tija na ufanisi katika utoaji huduma ikiwemo mizigo kupakuliwa kwa wakati.

Mgandilwa ametoa mwito huo leo Mei 26, 2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo amesema maboresho katika bandari hiyo yamegharimu takriban shilingi bilioni 429.

Kutokana na maboresho hayo, amesema yamefanya wilaya ya Tanga na mkoa wa Tanga kwa ujumla kuingia katika historia ya utoaji huduma za bandari ikiwa ni pamoja na meli kupaki kwenye gati.

“Tanga tumeingia katika historia ambapo kwa mara kwanza meli kuja kupaki kwenye gati hapa ambapo kwa miaka mingi meli zilikuwa zinapaki ndani ya maji umbali kilometa 1.7” amesema Mgandilwa

Nakuongeza "Hata zile gharama ambazo watu walikuwa wanazilalamikia za mipakuo (double handling) sasa hazipo tena. Ni wakati sasa wafanyabiashara kutumia fursa hii” amesisitiza Mgandilwa

Pia Mkuu wa Wilaya Mgandilwa, amewasihi wafanyabiashara kutojihusisha na magendo kwani athari za kufanya vitendo vya kimagendo ni kubwa lakini pia vyombo vya ulinzi na usalama katika kuyadhibiti magendo hayo viko macho.

“Serikali ya awamu sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa boti mpya kwa ajili ya kudhibiti magendo lakini pia vyombo vyetu vya ulinzi na usalama viko macho kuhakikisha kuwa hakuna magendo yanayoingia kupitia lango la wilaya yetu ya Tanga” amesema Mgandilwa

Kuhusu umuhimu wa kutumia bandari ndogo zilizorasimishwa na suala zima la udhibiti wa magendo, Mkuu huyo wa wilaya amesema anawaomba Watanzania, kuona umuhimu wa kutumia bandari ambazo ni rasmi.

"Kufanya magendo ni hatari, unaweza ukawa na mtaji wa shilingi milioni 5 au 6 ukifanya magendo na ukakamatwa unapoteza vyote hadi huo mtaji wako. Hakuna ulazima wa kupoteza mtaji wako wakati unaweza kufuata sheria na mambo yakaenda vizuri”

Kwa upande wake Ofisa Masoko Mwandamizi wa Bandari ya Tanga, Rose Tandiko amesema, mchakato wa urasimishaji wa bandari ndogo za Pangani, Kipumbwi na Mkwaja na Sahare umeleta matokeo chanya katika usimamizi wa bandari.

Hivyo kuwezesha mazingira ya kufanya biashara kati ya Mkoa wa Tanga na wilaya zake pamoja na maeneo ya visiwani kuwa rahisi, nafuu na yenye kuleta tija

Tandiko ameongeza kuwa, uwepo wa bandari hizi ndogo umechochea kasi ya ongezeko la mapato katika Mkoa wa Tanga. “Uwepo wa bandari ndogo zilizorasimishwa umeleta chachu ya kuongezeka kwa mapato katika Mkoa wa Tanga na.

"Pia kuwafanya wafanyabiashara kuwa huru katika shughuli zao kwani kabla ya urasimishaji wa bandari hizi zilikuwa zinatambulika kama bandari bubu” amesema Rose

Wakati huo huo mmoja wa wakazi katika bandari ndogo ya Sahare, Bwembe Hassan Idrisa ameeleza kuwa, kurasimishwa kwa bandari hiyo kumechochea ukuaji wa viapto vyao kwani wafanyabiashara wanaoshusha katika bandari hiyo wameongezeka.

Pia kumekuwepo na fursa ya ajira hususan kwa vijana kupatikana katika maeneo mbalimbali ikiwemo upakuaji wa mizigo na Uvuvi

Urasimishaji wa bandari ndogo unatajwa kuwa njia bora ya kukuza mapato ya serikali kwa kuweka mazingira salama kwa wananchi kwa ajili ya shughuli za ikiwemo usafirishaji wa mizigo.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) imepewa majukumu makubwa yanayotokana na sheria ya Bunge iliyoanzisha TPA. Sheria namba 17 ya mwaka 2004 inayosema kwamba kazi za TPA ni kuhakikisha inajenga, kuendeleza na kusimamia bandari zote nchini.

Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Hashim Mgandilwa akiongea na waandishi wa habari juu ya faida zilizopatikana kufuatia maboresho makubwa yaliyofanyika katika bandari ya Tanga Mei 26, 2023

Afisa Masoko Mwandamizi, Bandari ya Tanga, Rose Tandiko akiongea na waandishi wa habari kuhusu mchango wa bandari ndogo zilizopo katika Mkoa wa Tanga ambazo zimerasimishwa na namna zinavyochochea ukuaji wa mapatoMkazi wa Sahare, Bwembe Hassan Idrisa akiongea faida zinazopatikana kwa jamii inayozunguka bandari ndogo ya Sahare mara baada ya kurasimishwaMichuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...