Na Mwandishi Maalumu -Nigeria
UBALOZI wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Voice of Nigeria, umefungua Darasa la Kiswahili kwa wafanyakazi wa Voice of Nigeria.
Imeelezwa kwamba mafunzo hayo ni kwa ngazi ya awali kwa ajili VON kujiandaa kuimarisha Idhaa yao ya Kiswahili, yalifanyika Mei 9, 2023
Mafunzo yamefunguliwa na Balozi Benson Alfred Bana ambaye ni Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Nigeria na Mkurugenzi wa VON, Osita Okechukwu
Aidha, VON September 23, 2022 walisaini hati ya makubaliano na TBC, ambapo pamoja na mambo mengine kwa ajili ya kushirikiana katika Kutangaza Kiswahili.
Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Dk.Benson Bana akizungumza wakati wa ufunguzi wa darasa la Kiswahili kwa wafanyakazi wa Voice of Nigeria.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...