Dah! Siku zinayoyoma jamani. Yaani inaonekana  watoto wa mastaa maarufu duniani hawa walikuwa wachanga juzi juzi tu, lakini sasa watoto hawa mashuhuri wamekua wakubwa huku wakifaidika na fursa za kipekee katika maisha yao. Baadhi yao wamekua sana hivi sasa kiasi kwamba unaweza usiwajue kabia. Na wengine wamejijengea umaarufu wao wenyewe katika ulimwengu pasina kutegemea umaarufu wa wazazi wao. 

Hebu wacheki baadhi yao hapa chini...

 

JADEN "KARATE KID" - Wazazi: Will Smith, Jada Pinkett Smith

Ah, Jaden Smith. Wakati hayuko katika kufanya muziki na kucheza filamu na baba yake, unaweza kumkuta  akifurahia muziki katika mafestivali ya muziki ya Los Angeles na kudai anaweza kusafisha nyota za watu. Lakini angalau hapigi  kofi wachekeshaji katika matangazo ya moja kwa moja ya televisheni – kama alivyofanya baba yake Will Smith aliyemzabua kibao wakati wa tuzo za Oscar mwaka jana.

SISTINE  "RAMBO" STALLONE - Wazazi: Sylvester Stallonenna Jennifer Flavin

Akifuata nyayo za baba yake, Sistine Stallone ni mwigizaji ambaye alianza kazi yake katika filamu ya kutisha ya mwaka 2019 "47 Meters Down: Uncaged". Pia amepata umaarufu kama  modo wa Instagram, akiwa na zaidi ya wafuasi milioni moja wanaopata stori za  maisha yake ya anasa. Sistine pia anafanya kazi kama modo wa  kuonyesha umbo lake zuri.

PARIS JACKSON- Wazazi: Michael Jackson, Debbie Rowe 

Huyu ni Mtoto wa pili (na pekee wa kike) wa Michael Jackson na Debbie Rowe, Paris Jackson, hivi karibuni amefuata nyayo za baba yake na kujihusisha na muziki. Ila mmmhh.. kumudu kurithi mambo ya baba yake wakati baba yake huyo ni mfalme wa pop duniani yeye mwenyewe ni changamoto kubwa.

PATRICK SHWARZENEGGER - Wazazi: Arnold Schwarzenegger, Maria Shriver

Kama baba yake “Commando” Arnold Schwarzenegger, Patrick alifuata nyayo za taaluma ya uigizaji. Aliaanza na filamu ndogo ndogo  hadi alipopata nafasio ya muigizaji kiongozi (Stering)   katika filamu kali ya mwaka 2018 "Midnight Sun". Mwaka 2016, alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Biashara cha USC Marshall. Patrick alisaini mkataba na IMG Models ili kushiriki katika kampeni na kukuza kampuni  yake ya nguo.

  

CHRISTIAN P DIDDY  - Wazazi: Sean Combs, Kim Porter.

Wazazi wa Christian Combs ni rapa Sean "P Diddy" Combs na marehemu Kim Porter. Kama mtu mzima, Christian amejishughulisha na uigizaji na rap, akifanya maonyesho katika matukio makubwa kama Spotify's Dipset Reunion na Rolling Loud Music Festival. Amekuwa modo wa kutangaza  kwa bidhaa kubwa kubwa kama Dolce na Gabbana, hasa wakati wa kampeni yao ya matangazo ya 2018.

JULIE "SCARFACE" Wazazi: Al Pacino, Jan Tarrant

Badala ya kujihusisha na uigizaji, Julie, binti ya muigizaji maarufu wa sinema kali kama vile “Scarface” Al Pacino, aliamua kujihusisha na utengenezaji wa filamu. Amejishindia tuzo kibao katika matamasha ya filamu, pamoja na Hollywood Gold Awards, Indie Short Fest, na Hollywood Reel Independent Film Festival. Pia anajitokeza yeye kama yeye mwenyewe katika filamu  inayokuja karibuni.

SIMONE - Wazazi: Dwayne Johnson, Dany Garcia

Kama alivyo baba yake Dwayne Johnson, Simone ni bingwa wa mieleka. Ingawa amefanyiwa upasuaji wa goti mara kadhaa, Simone anafanya mazoezi kwa bidii na alisaini mkataba na WWE mwaka 2020 akiwa na umri wa miaka 19 tu. Pia anashiriki picha za umodo  kwenye Instagram, akionyesha kwamba ana mpango wa akiba ikiwa njia moja ya kazi haitafanikiwa

 

COLIN- Wazazi: Tom Hanks, Samantha LewesIngawa kuwa na Tom Hanks kama baba yake kunaweza kumpa fursa nzuri, Colin amethibitisha uwezo wake katika tasnia ya uigizaji. Alishinda jukumu lake hilo la kwanza katika miaka ya 90 na ameendelea kufanya kazi katika filamu na vipindi vya runinga kwa miongo miwili iliyofuata. Wataalam wamempa sifa nyingi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...