MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Mhe. Omary Kumbilamoto akizungumza jambo mbele ya Wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa simu aina ya Tecno Camon 20 Series, uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Kumbilamoto amewaomba Watanzania kuwa na imani na simu za Tekno ambazo wamekuwa wakizizindua kwani wamekuwa wakileta simu bora na imara kwa matumizi.


MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Mhe. Omary Kumbilamoto ameipongeza Kampuni ya Vodacom kushirikiana na Tekno Tanzania kuja na simu aina ya Tecno Camon 20 Series ambazo ni bora kwa matumizi ya mawasiliano na internet.

Ametoa pongezi hizo mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam katika hafla ya uzinduzi wa simu hiyo, ambapo amewaomba Watanzania kuwa na imani na simu za Tekno ambazo wamekuwa wakizindua kwani wamekuwa wakileta simu ambazo ni bora na imara kwa matumizi.

"Tekno wamekuwa wakijitahidi kuleta simu bora na imara, mimi pia ni mpenzi wa simu za Tekno na hapa nilipo natumia simu ya Tekno, naamini katika ubora wao pia,hivyo nawaomba wananchi wa Dar es Salaam kutumia simu za Tekno kufurahia huduma zilizo bora kabisa". Amesema

Kwa upande wake Meneja Bidhaa za Intaneti - Vodacom Tanzania Samwel Mlole amesema kila Mtanzania ambaye atanunua simu hiyo atazawadiwa 95Gb bure za internet kwa mwaka mzima kwa maana atakuwa anapata 8Gb kila mwezi kwa muda wa miezi 12.

"Ofa hii itampelekea Mtanzania huyu kuweza kupata taarifa mbalimbali na kuweza kujua na kuona faida na uzuri wa hii simu katika angle mbalimbali". Amesema Bw.Mloe

Nae Meneja wa Mafunzo kutoka Tekno Tanzania Bi. Joyce Kaswalala amesema simu hiyo inasifika kuwa na camera nzuri na zimekuja na processor kubwa ambayo inasifika kwa utendaji mzuri wa kazi katika simu.

"Simu hii kwa upande wa Camera inasifika kuchukua picha wakati wa usiku lakini pia picha na video ambazo ziko stable kwasababu imekuja na kitu kinaitwa Sensa shift yenyewe kazi yake kubwa ni kustablize video ambazo zipo katika movement". Amesema

Meneja Bidhaa za Intaneti - Vodacom Tanzania Samwel Mlole akimueleza jambo MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Mhe. Omary Kumbilamoto namna simu hizo zilivyo imara,bora na za kisasa kabisa

Meneja Bidhaa za Intaneti - Vodacom Tanzania Samwel Mlole akitoa ufafanuzi namna Kampuni ya Vodacom Tanzania inavyoshirikiana na Wadau wengine katika mawasiliano,wakati wa hafla fupi uzinduzi uzinduzi wa simu aina ya Tecno Camon 20 Series,uliowakutanisha wadau mbalimbali wa bidhaaa hizo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...