Na Mwandishi Wetu, Same

MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni amewaonya wananchi wanaohujumu miundombinu ya maji katika wilaya hiyo kuacha mara moja kwani wanarudisha nyuma maendeleo.

Ametoa onyo hilo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Hedaru na Mabilion ambapo amesema yoyote atakaye bainika kufanya hujuma katika miundombinu ya Miradi ya Maji ambayo inasimamiwa na (RUWASA) atachukuliwa hatua kali.

"Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ametoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo hapa nchini ili wananchi waweze kunufaika, " amesema Kasilda.

Aidha amemuagiza Meneja wa RUWASA Abdallah Ally kuendelea kutoa elimu kwa wananchi pindi wanaposambaza mabomba ya maji huku akimtaka Diwani wa Kata ya Hedaru John Ali kuhakikisha vyazo vyote vya maji vinatunzwa ili maji yasambazwe kwa wananchi wote wa Kata hizo mbili

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Hedaru amempongeza Mkuu wa wilaya kwa kazi kubwa anayoifanya kuendelea kutatua kero na migogoro kwa wananchi wa wilaya ya Same na kuahidi kushirikiana naye kwenye kuleta maendeleo katika kata ya Hedaru na mabilion ambapo wananchi zaidi ya 5000 Katika kijiji cha kijumo watanufaika na mradi huo unaotekelezwa na RUWASA


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...