Na Jane Edward, Arusha

Makamu wa Rais , Dk .Philip Mpango amezitaka Taasisi za fedha nchini kutoa mikopo ya riba nafuu kwa makundi mbalimbali wakiwemo wachimbaji wadogo wa madini,wavuvi, wakulima na wafugaji ili waweze kupiga hatua katika kiuchumi.

Akizungumza jijini Arusha wakati wa kufungua semina kwa wanahisa wa benki ya CRDB inayofanyika katika ukumbi wa mkutano wa Aicc jijini Arusha.

Amesema taasisi nyingi za fedha zimekuwa zikitoa mikopo ya riba kwa asilimia 9 ,hivyo aliomba kupunguza zaidi chini ya asilimia 9 ili kuwapa fursa wafanyabiashara wadogo na wananchi waliopo vijijini kuweza kupata huduma za mikopo yenye riba nafuu

Pia ameyataka mabenki kuzingatia ufanisi katika utendaji kazi ikiwemo kuongeza gharama za uendeshaji katika matumizi ya Tehama , sambamba na kuhakikisha hakuna mikopo chechefu mipya na kuzingatia ukomo wa asilimia 5 uliowekwa na benki kuu ya BOT.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya benki ya CRDB, Dk Ally Laay ameomba serikali kupitia wizara ya elimu kuandaa mitaala maalumu wa kuwafundisha wanafunzi umuhimu wa kuwekeza katika Hisa ili kuwapa elimu ya fedha na matumizi sahihi.

Ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuwekeza kwenye hisa kwani kama Taifa kuna mwako mdogo sana ya uwekezaji katika maswala ya Hisa .

Awali Mkurugenzi wa benki ya CRDB, Abdulmajjid Nsekela amesema semina hiyo ni utaratibu waliojiwekea kila mwaka wa kutoa elimu ili kuhamasisha idadi ya wanahisa ambayo ni chache kwa mabenki mbalimbali hapa nchini kutokana na kutokuwa na elimu ya fedha ndio maana kumekuwa na utaratibu wa kutumia semina ya wanahisa.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Philip Mpango akihutubia Mkutano wa wanahisa jijini Arusha.

Mwenyekiti wa bodi Bank ya CRDB Dkt  Ally Laay akizungumza katika mkutano huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bank ya CRDB  Abdulmajjid Nsekela akielezea mafanikio ya Bank hiyo kwa Mgeni rasmi.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Philip Mpango  akimsikiliza mjasiriamali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...