Na John Walter-Manyara.

Mradi wa ujenzi wa bomba la Mafuta Ghafi Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima, Uganda hadi Chongoleani, Tanga unaendelea kushika kasi ambapo waguswa 475 mkoani Manyara mpaka sasa wamelipwa fidia kiasi cha shilingi Bilioni 2.3.

Akizungumza kwenye kikao cha tathmini kuhusu mradi huo mkubwa unaopita pia katika mkoa wa Manyara wilaya za Mbulu,Kiteto na Simanjiro, Mwakilishi kutoka Wizara ya Nishati Yovin Uisso amesema kwa sasa kinachoendelea ni kulipa fidia kwa wananchi wanaopisha mradi huo na kuandaa vituo vikubwa na vidogo vitakavyotumika kwenye ujenzi.

Mratibu wa tathmini na malipo EACOP Mussa Mlupilo amesema waguswa katika mradio huo ni 9,508 na hadi sasa zoezi la kutia saini limefika asilimia 98 huku mkoa wa Manyara kwenye wilaya tatu ikiwa na waguswa 475, ambapo kati yao 462 wametia Saini.

Zoezi linaloendelea ni kutoa notisi watu kuhama ambapo mwisho wa kuhama kwa watu wote ni Mei 6,2023.Mradi huo utapita katika Mikoa 8 ambazo ni Kagera, Manyara, Geita, Shinyanga, Dodoma, Singida, Tanga, Tabora katika Wilaya 24.

Katibu tawala mkoa wa Manyara Karolina Mthapula, amesema wataendelea kufuatilia migogoro iliyopo kwenye maeneo ambayo mradi huo utapita ili kuondoa usumbufu wowote unaoweza kujitokeza na kuchelewesha mchakato wa ujenzi wa bomba hilo.

Bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima, Uganda hadi Chongoleani, Tanga kwa upande wa Tanzania litakuwa na urefu wa kilomita 1,147 ambapo inatarajiwa kuzalisha ajira elfu 10 hadi elfu 15 kwa Watanzania.Hadi kukamilika kwake, mradi huo unatarajiwa kugharimu dola za Kimarekani bilioni 5.1.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...