Makamu Mkuu wa shule ya Sekondari ya Baobab Alphonse Kamisa  akiwakaribisha wafanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) waliofika shuleni hapo kwa ajili ya kutoa elimu na  kuwahamasisha wanafunzi hao kujiunga na masomo ya Uhasibu watakapomaliza masomo yao.
Afisa Masoko na Mawasiliano wa NBAA, Magreth Kageya akitoa elimu kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Baobab iliyopo Mapinga, Bagamoyo mkoani Pwani.
Mwalimu wa Shule ya Sekondari Baobab  Lucas Lubango akizungumza kwa wanafunzi madhumuni ya Wafanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) kufika shuleni hapo.
Mfanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Sawa Ngendabanka akitoa elimu pamoja na kuwahamasisha wanafunzi kujiunga na masomo ya Uhasibu watakapomaliza masomo ya Sekondari katika Shule ya  Sekondari ya Baobab iliyopo Mapinga, Bagamoyo mkoani Pwani.
Mfanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Sawa Ngendabanka akisikiliza swali alilokuwa anauliza mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Baobab wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na NBAA.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Baobab wanaosoma masomo ya Biashara wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yanatolewa na wafanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) waliofika kutoa elimu shuleni hapo Mapinga, Bagamoyo mkoani Pwani.
Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Baobab Stephen Gervas Mahundi  akitoa neno la shukrani kwa wafanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) waliofika shuleni hapo  Mapinga, Bagamoyo mkoani Pwani kutoa elimu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...