Na Pamela Mollel,ARUSHA

MKAGUZI wa Jeshi la Polisi,Ally Babu amefunga ndoa ya kijeshi na mchumba wake,Selani Sumai na tukio hilo, lilikuwa kivutio kwa watu walioshiriki kutokana na kufanyika kwa matukio mbalimbali ya kijeshi ikiwamo kupigwa kwa gwaride la nguvu wakati wa sherehe hiyo.

Ndoa hiyo ya kijeshi ilifungwa mwisho ni mwa wiki jijini Arusha na kuhudhuriwa na viongozi waandamizi wa Jeshi hilo na viongozi wa Serikali.

"Kwa kweli imekuwa siku muhimu katika maisha yangu kwa kufanya jambo la kipekee ambalo linafungua njia na taswira nyingine kwa sisi wawili,"alisema Babu

Alisema kama ilivyokuwa kwa binadamu wengine Mungu amependa wawili hao kuwa kitu kimoja na kwenda kuanzisha mchakato wa maisha mapya ambayo yatakuwa sehemu ya kuunda familia bora na imara itakayokuwa ya mfano katika Jamii.

"Tuna mshukuru Mungu kwa kufanikisha shughuli yetu ya ndoa hii kufungwa nina furaha na tunatarajia kuishi maisha ya furaha na upepo ambayo yatakuwa mfano kwa wengine kuiga,"alisema Sumai






 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...