Njombe

Madiwani halmashauri ya mji Njombe wameridhia kutenga maeneo ya ujenzi wa Chuo Kikuu kwenye mji huo ikiwa ni kilio cha miaka mingi cha wananchi mkoani Njombe kutokana na kutokuwa na Chuo Kikuu na kupelekea wanafunzi kwenda mikoa mingine kwa ajili ya elimu ngazi ya juu.

Wakizungumza katika mkutano wa baraza la Madiwani baadhi ya madiwani akiwemo Ulriki Msemwa diwani wa Luponde,Honolatus Mgaya diwani wa Makowo,Alatanga Nyagawa wa Njombe mjini na Anjela Mwangeni wa viti maalum wameonesha kiu yao ya kutaka kujengwa kwa chuo kikuu ili kukuza mji na mkoa huo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji Njombe Erasto Mpete amesema jitihada mbalimbali za kuhakakikisha halmashauri ya mji Njombe inakuwa manispa nikuhakikisha vyuo vikuu na vya kati vinajengwa.

"Madiwani tumeidhinisha kutenga maeneo ya ujenzi wa chuo kikuu na vyuo vya kati kwa kuwa ajenda ya manispaa ni ya kimkoa,tunaamini chuo kikuu kinajengwa ndani ya halmashauri ya mji Njombe ili lengo la kuelekea kuwa manispaa liweze kutimia"Erasto Mpete mwenyekiti Njombe TC

Amos Luhamba Afisa Aridhi Halmashauri ya mji njombe kwaniaba ya Mkurugenzi amesema maeneo ya kujenga chuo kikuu tayari yashatengwa ambayo ni Nundu,Uwemba,Ihalula, na eneo lililokaribu na Shule ya Sekondari Njombe (NJOSS).



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...