Na Mwandishi Wetu

KUMEKUWEPO na majadiliano yanayoendelea katika nchi za Afrika ikiwemo Tanzania na sehemu kubwa ya majadiliano hayo yanahusu namna nzuri ya kuendeleza mbegu za asili ambazo zinatumiwa na wakulima.

Hiyo inatokana na uwepo wa dalili mbalimbali zinaonesha mbegu za asili za wakulima kama hazitatafutiwa njia sahihi ya kuzitunza na kuzilinda itafika mahali ambako hakutakuwa na uhuru wa chakula kwani uhuru wa chakula unatokana na uwepo wa mbegu za uhakika kwa wakulima.

Katika kunogesha majadiliano kuhusu mbegu za asili za wakulima tayari Shirika lisilo la kiserikali la Afsa la nchini Uganda limekuja na mapendekezo kadhaa yanayoonesha kuwa yakifuatwa na kutekelezwa upo uwezekano wa mbegu za asili za wakulima kuendelea kuwepo na kutumika.

Hata hivyo mapendekezo hayo yamesababisha wadau wakubwa katika sekta ya kilimo nchini Tanzania kutoa maoni na ushauri wao kuhusu uendelezwaji wa mbegu za wakulima kwa maana ya mbegu za asili.

Mratibu wa Taasisi isiyokuwa ya Kiserikali ya TABIO Abdallah Ramadhan Mkindi anatumia nafasi hiyo kufafanua mapendekezo ya AFSA na kwa mtazamo wake mapendekezo hayo yamekuja wakati muafaka.

“Tumewaita kuja kuwashirikisha kuhusu mfumo pendekezwa ambao umeandaliwa na ndugu zetu wanaoitwa Afsa ambao ni mtandao wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kwa ngazi ya Afrika na wanafanya kazi katika nchi mbalimbali duniani …

“Katika kuhamasisha masuala ya kuwa na uhuru wa chakula katika bara la Afrika, na uhuru wa chakula unapatikana pale ambapo uhuru wa mbegu unakuwepo , mmojawapo ya nyanja ya maeneo muhimu ya kuzungumzia uhuru wa mbegu ni katika mfumo wa mbegu unaomilikiwa na wakulima.

“Sasa mfumo wa mbegu zinazomilikiwa na wakulima tafiti zimefanyika katika ngazi ya Afrika zinaonesha karibia asilimia 80 ya mbegu ambazo wakulima wamezitumia zinatokana na mfumo wa mbegu zinazomilikiwa na wakulima.

“Kwa hapa Tanzania tafiti zimefanyika na zinaonesha mfumo huo unachangia zaidi ya asilimia 60 kwa baadhi ya mazao, na mazao mengine kwa asilimia asilimia 90 , na yapo mazao yanayotokana na mfumo huo kwa asilimia 100.”

Mkindi amesema kwa hiyo unakuta mfumo huo unategemewa kama chanzo cha mbegu kwa wakulima hasa wadogo wadogo, sasa pamoja kwamba huo mfumo unachangia kwa kiasi kikubwa cha upatikanaji wa pembejeo ambazo wakulima wanazitumia lakini haujawekewa mkakati wa kutosha ya kulinda mifumo iliyopo ili isipotee

“Hata katika sera ya kilimo inaonesha huu mfumo haujatajwa wazi kama ni mojawapo ya chanzo cha pembejeo ambazo wakulima wanazitegemea lakini pia kwenye sheria yetu ya mbegu ya mwaka 2003 na sheria ya mwaka 2014 mfumo wa mbegu za mkulima haujatajwa.

“Kwasaababu huo mfumo kwenye sera haupo , kwenye sheria haupo , hivyo inakuwa ngumu kwa Serikali kuwekea mipango au kanuni za kusimamia . Sasa huo wenzetu wa AFSA wameandaa huu mfumo pendekezwa wa kusimamia na kutambua na kuhamasisha mfumo mbegu zinazomilikiwa na wakulima na kulinda viumbe hai ili usipotee.”

Ameeleza hivyo wao wanaona mfumo kama huo ambao chanzo kikubwa cha mbegu ambazo wakulima wanazitegemea kwa ajili ya kuzipanda kutoka msimu mmoja mpaka mwingine , mfumo uliopendekezwa na AFSA basi Serikali na wadau nao waupitie ili waone.

Lengo ni kutambua kwa kiasi gani na Watanzania wanaweza kuandaa mfumo wa kusimamia mbegu za mkulima ili zisipotee.

Akizungumzia kuhusu athari za kupotea kwa mbegu za asili?Mkindi anasema mbegu za mkulima zikipotea athari yake ni kubwa, kwanza kwenye upatikanaji wa aina ya vyakula ambavyo walaji wanavitegemea , wanavitaji huku akifafanua sasa hivi kuna changamoto ya magonjwa mengi yasiyoambukizwa ambayo yameripotiwa na takwimu ziko na kiulimwengu zinaonesha hali sio nzuri

“Kuna magonjwa mengi yasiyoambukizwa , utaambiwa kisukari, moyo , presha, na mengine ambayo yanatokana na ulaji mbovu au kula vyakula ambavyo sio salama, kwa hiyo mfumo huo wa mbegu za wakulima unawawezesha wakulima na walaji kupata vyakula ambavyo kwa afya kwa maana ndani yake vinalishe lakini pia kujitosheleza kwa chakula.

“Tafiti ambazo zimefanyika maeneo mbalimbali hapa Tanzania hasa mikoa ya nyanda za juu kusini inaonesha pamoja na ile mikoa inazalisha chakula kingi hasa mahindi, lakini bado hiyo mikoa iliongoza kwa kuwa na utapia mlo kwa watoto wadogo.”

Hivyo hali hiyo inaonesha kuna tatizo aidha kukosa vyakula vyenye lishe kwasababu kula chakula cha aina moja na kukosekana kwa wigo mpana wa vyakula ambavyo watoto wanaweza kula

Ametaja athari nyingine ni upotevu wa viumbe hai vya mbegu za mkulima na Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zinautajiri mkubwa wa viumbehai na hata duniani kwa ujumla inashika nafasi za juu.

Hivyo hizo mbegu zikipotea maana yake tunapoteza na viumbehai na hizo mbegu ni chanzo kikubwa cha kupata vinasaba ambavyo watafiti wanavitegemea kwa ajili ya kuboresha mbegu.

“Kwa hiyo hizi mbegu zikipotea inamaana tunapoteza wigo au fursa ama vyanzo vya upatikanaji wa mbegu ambazo wakulima au watafiti wetu wanazihitaji kwa ajili ya kufanyia tafiti za kuboresha mbegu ambazo zinahitajia kwa wakulima na masuala mengine mengi ya kiuchumi, kijamii, kimila na desturi ambazo yameambana na hizo mbegu.

Kuhusu uanzishwaji wa benki ya mbegu za mkulima,anasema kama neno lenyewe benki ni sehemu ya kuhifadhia vitu, kwa hiyo benki za mbegu zikianzishwa na wale wakizisimamia wakapewa maarifa yanayohitajika kusimamia hizo mbegu zitakuja kupatikana.

“Lakini kuanzisha benki bila maarifa utaziweka tu kwenye hiyo benki lakini zitakufa kwasababu unapoweka kitu kwenye benki lazima ujue ili mbegu ibaki kuwa hai inahitajika kitu gani.Unaweza weka kwenye benki lakini baada ya muda ukienda kupanda hazioti.

“Kumbe hukuwa na maarifa kwa hiyo lazima benki hizo zikianzishwa wale wanaozimamia wapewe elimu na maarifa yanayostahiki kusimamia benki hizo za mbegu na ikifanyika hivyo itakuwa sehemu rahisi ya wakulima kupata hizo mbegu na hizo benki za mbegu itakuwa chanzo cha kufikiwa kwa mahali walipo wadau wanaozihitaji.

“Na pia mkulima anaweza kuzitumia kwa kuzalisha kwa ajili ya wengine wanaohitaji wakazipata, pia wadau kama vituo vya utafiti wanapozihitaji kwa ajili ya utafiti nadhani benki za mbegu ni sehemu sahihi ambapo wanaweza kuzipata kwa ajili ya matumizi ya hizo mbegu.”

Alipoulizwa iwapo benki za kuhifadhi mbegu zimeanzishwa, amejibu tayari zimeanzishwa na zinaendelea kuanzshwa kwenye mikoa tofauti tofauti kwani kumekuwepo na jitijitahada za mashirika mbalimbali yasiyokuwa ya kiserikali ambayo yaanzisha benki za mbegu.

“Kwa mfano katika wasilisho ambalo tumelifanya wakati tumekutana na kamati ya Bunge ,Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo tulianisha kwamba kuna benki nyingi ambazo zimekwisha aanzishwa mfano katika mkoana Arusha na hiyo inatokana na jitihada zinazofanyika

“Benki za mbegu za jamii 10 zimeanzishwa mkoani Arusha,Morogoro benki tatu, Lindi na Mtwara kuna benki saba, Shinyanga kuna benki mbili, Songwe benki mmoja na bado kuna zingine zinaendelea kuanzishwa.

“Kwaasababu wakulima na jamii wamehamasika katika kuzianzisha hizo benki na baadhi hizo mbegu zinasimamiwa kwa karibu na maofisa ugani na kituo cha taifa cha kuhifadhi vinasaba kilichopo Arusha.”

Kwa upande wake Paul Chileo ambaye ni Ofisa Ufuatiliaji, Tathimini na Ushawishi kutoka Taasisi ya Kilimo Endelevu(TOAM) amesema dunia kwa sasa inataka maendeleo endelevu na kilimo kinabeba watu wengi na hasa kwetu Afrika.

“Kwa hiyo bila kuwa na kilimo endelevu cha kwanza tunakuwa na tatizo kubwa sana na dunia ikiwemo Tanzania tunataka kuboresha mifumo ya chakula na kama mnajua kuna mkutano mkubwa unaohusu masuala ya kilimo, huwezi kubadilisha mfumo wa chakula…

“Na ukawa endelevu bila kuwa na mjadala kwenye mbegu na hasa bila kuchukua hatua kwenye mbegu ambazo zinamilikiwa na wakulima. Kwa hiyo lile swali la kwanini hizi mbegu, kwanza zina mchango mkubwa kwenye usalama wa chakula,”amesema.

Ameongeza pili kwenye kuhakikisha lishe inapatikana kwani inaelezwa kuna mikoa ambayo inazalisha zaidi lakini ndio inayoongozwa kwa kuwa na utapia mlo.

“Ndio maana siku hizi watu wanatafuta dawa za nguvu za kiume lakini kuna vyakula ambavyo ni zaidi ya dawa za hizo , kwa hiyo kitu cha kwanza kutambua watunga sera , haya mapendeko ya Afsa yanaleta mapendekezo ambayo yanatufanya tuwe na mifumo ya chakula endelevu.

“Ukiangalia mapendekezo yote yanalengo la kuleta mfumo wa chakula endelevu na kuna changamoto kubwa kwenye mifumo yetu ya chakula ambapo watalaam wanasema inabidi tuondoe ukoloni mamboleo na Afrika kwamba tunafikiria tunachangamoto ya utapia mlo lakini suluhu haitoki ndani na wakati mwingine inapotoka nje inakuwa sio endelevu au sio ambayo inaleta mabadiliko yanayotakiwa.

“Mfano tuna mbegu ambazo zinaweza kutusaidia kutatua tatizo la lishe na utapia mlo lakini ukisikiliza mbegu zinazopigiwa chapua hazileti suluhisho la kuzalisha chakula ambacho kitakuwa kina lishe, tunachangomo kubwa sana.”

Ameongeza unakuta chakula kinachozalishwa inabidi kikafanyiwe uchunguzi, lakini kuna mbegu ambazo zinaweza kuzalisha na zikatoa mchango mkubwa kwenye kutatua tatizo la lishe kwa hiyo ukiangalia yale mapendekezo ya AFSA kwa kiwango kikubwa yanataka kuja na suluhu ya kudumu

Ametoa mfano wanataka kutengeneza kamati ya kitaifa ambazo zitatambua mbegu zetu zipo na zipo kwenye hali gani na zinaendelezwaje.Baada ya hapo kuzilinda na kuziendeleza.Hivyo sasa wanakuja na mapendekezo ya mikoa lakini kuna maeneo ya kiasili.

Hivyo anasema ni vizuri kushirikisha benki za asili ili katika mfumo huo wa kuzilinda na kuziendeleza wakulima washiriki kikamilifu na usiwe mfumo wa watalaamu peke yao na wakulima peke yao.“Tunachotaka ni kuona mtandao mzima wa wakulima unashirikishwa na kupewa kipaumbele kwenye vituo vya utafiti.”

Mratibu wa Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya TABIO Abdallah Mkindi akiwa ameshika chapisho la jarida la mapendekezo kuhusu utunzaji wa mbegu za mkulima .Chapisho hilo la mapendekezo limeandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la AFSA



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...