Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

WANANCHI wa Jimbo la Kalenga katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kupitia Wizara wa Maji kwa usimamizi wa Bodi ya Bonde la Rufiji za kukamilisha ujenzi wa bwawa la kufuga samaki lililopo Kata ya Masaka.

Akizungumza Mei 29,2023 mbele ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye alifika kwenye Mradi wa bwawa hilo kwa ajili ya uzinduzi wa ufugaji samaki awamu ya kwanza , Ofisa Uvuvi Wilaya ya Iringa Kelvin Ndege amesema halmashauri imekuwa ikifanya juhudi ya uhamasishaji wananchi kujikita katika shughuli za ufugaji samaki.

“Tunapenda kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ametuletea fedha zaidi ya Sh.bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la kuhifadhia maji katika kipindi chote cha majira ya mwaka hasa kiangazi kwa ajili ya shughuli za kibinadamu , kilimo cha umwagiliaji, matumizi ya majumbani na ufugaji wa samaki.

“Kumekuwepo na juhudi za uhamasishaji wa wnanchi katika ufugaji wa samaki katika halmashauri ya Iringa yenye mabwawa ya samaki 350 na mabwawa ya watu binafsi 221 na mabwawa 45 kupitia taasisi tofauti zikiwemo za mashirika ya dini na kuna mabwawa mengine ya kijiji.

“Bwawa la Masaka limejengwa kwa usimamizi wa Wizara ya Maji, chini ya Mamlaka ya Bonde la Mto Rufiji , kwa nafasi hii pia tunamshukuru Waziri wa Maji Juma Aweso lakini Mkurugenzi wa Bodi ya Maji kwa kuhakikisha ujenzi wa bwawa hilo unakamilika kwa wakati.

“Bwawa hili linapatikana Kata ya Masaka iliyopo kwenye Halmashauri ya wilaya ya Iringa na litanufaisha vijiji vinavyozunguka bwawa hilo kwa ujumla , bwawa la masaka lina ukubwa wa kilometa za mraba 7.33 na lina uwezo wa kuhifadhi ujazo wa maji zaidi ya lita ya 400,000 na mahitaji ya wananchi ni zaidi ya mita za ujazo 300,000 .

“Hivyo kuwa na uhakika wa kupata maji katika vijiji vya maeneo hayo kwa mwaka, na linakwenda kuhudumia wananchi zaidi ya 10,000.Tunakushuku Katibu Mkuu wa CCM kwenda kuzindua ufugaji wa samaki katika mabwawa kwa awamu ya kwanza na siku chache tunakwenda kuunda bodi kwa jitihadaza za Rais.Bodi hiyo itawezesha wananchi kufaida na rasilimali zinazokwenda kuwekwa kwenye bwawa hilo,”amesema Ndege.

Aidha amesema bwawa hilo lina uwezo wa kupata samaki milioni 1368.72 na hiyo ni kwa awamu ya kwanza na amemhakikishia Katibu Mkuu wataendelea kupata samaki ili kufikia malengo ya mwezi kwa bwawa kupata samaki kama walivyoeleza hapo juu.

“Bwawa hili kwa wananchi wa Kata ya masaka litawawezesha kuboresha lishe na kipato cha mtu mmoja mmoja , kuongeza kipato kwa jamii, kuongeza ajira kwa vijana watakaojishughulisha na shughuli za uvuvi , usafirishaji na biashara ya samaki.

“Katibu Mkuu tunaomba kuchukua nafasi hii kuwataja wadau wa maendeleo ambao wamejumuika nasi katika nyanya mbalimbali akiwemo Mbunge wa jimbo la Kalenga Jackson Kiswaga ambaye amekuwa akijitolea.

“Pia diwani Methew Banyagwa ambaye kwa jitihada zake binafsi amechangia kukamilika kwa mradi huu wa bwawa la samaki pamoja na wawekezaji wengine ambao kwa namna moja au nyingine wamechangia kukamilika kwa ujenzi wa mradi huu.


Baadhi ya Wanachama na wananchi wa kata ya Masaka wilayani Iringa wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo mara baada ya kuuzindua mradi huo wa ufugaji samaki katika bwawa la maji lililojengwa katika kata ya Masaka wilayani Iringa kwa gharama ya Sh bilioni 1.5.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akishiriki kupanda vifaranga vya samaki elfu tatu katika mradi wa ufugaji samaki bwawa la Masaka.

Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya kikazi mkoani Iringa akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Haji Ussi Gavu pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akimsikiliza Ofisa Uvuvi Wilaya ya Iringa Kelvin Ndege namna ya kupandikiza vifaranga vya samaki 3,000 kwenye bwawa hilo kabla ya kuuzindua mradi huo wa ufugaji samaki katika bwawa la maji lililojengwa katika kata ya Masaka wilayani Iringa kwa gharama ya Sh bilioni 1.5.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo pamoja na viongozi wengine wakishiriki kukata utepe kwa pamoja kuashiria uzinduzi mradi wa kupandikiza vifaranga vya samaki 3,000 kwenye bwawa la maji lililojengwa katika kata ya Masaka wilayani Iringa kwa gharama ya Sh bilioni 1.5.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...