-Ni ujenzi wa barabara ya Kilometa moja kuelekea kituo cha Afya Ifingo

Siku moja baada ya Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo kuagiza ujenzi wa kilometa moja ya barabara inayoenda Kituo cha Afya cha Ifingo, Mjini Mafinga Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (Tarura) wameanza kutekeleza.

Chongolo alitoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko ya wananchi na ombi kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Mafinga, Cosato Chumi aliyedai ikiwa barabara hiyo itachongwa itapunguza usumbufu mkubwa wanaokukumbana nao wananchi kuelekea kituoni hapo kupata huduma.

Kutokana na hali hiyo, Chongolo alitoa saa 24 kwa Tarura kuanza kutengeneza barabara hiyo jambo ambalo limeanza kutekelezwa.

Jana, gleda lilishuhudiwa likiendelea na kazi kwenye barabara hiyo muhimu kwa wananchi wanaohitaji kupata huduma kwenye kituo hicho cha Ifingo.

Chongolo yupo Mkoani Iringa kwa ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM, kuhamasisha uhai wa Chama ngazi za mashina pamoja na kusikiliza na kutatua kero za wananchi, huku maagizo mbalimbali anayotoa yakiendelea kutekelezwa.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...