WAZAZI nchini ambao watoto wao wamehitimu kidato cha sita kwa mwaka 2023 wametakiwa kuhakikisha wanaendelea kuweka uangalizi kwa watoto wao katika maadili wanapoelekea kwenye masomo ya Vyuo vikuu.

Wito huo umetolewa jana tarehe 20/5/2023 na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dk.Aneth Komba katika mahafali ya 22 ya Kidato cha Sita ya shule ya Sekondari ya Loyola ya Mabibo jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa, Wanafunzi hao wanapaswa kuendelea kuangaliwa hasa kwenye masuala ya malezi ili waweze kufikia malengo yao ya maisha.

"Wazazi kazi yetu ya kulea haijaishia hapa, tuendelee kuwafuatilia watoto wetu ili waendelee kusoma na kufikia malengo yao "amesema Dk.Komba.

Aidha, Akijibu hotuba iliyotolewa na Mkuu wa shule ya Loyola, Padri Martin Wawelu kuhusiana na rasimu za Sera na Mitaala, Dk.Komba ameeleza kuwa maoni yote ameyapokea na kuwa yatafikishwa katika maboresho ya rasimu hizo na kueleza kuwa maoni yanaendelea kutolewa na kupokelewa hadi tarehe 31/5/2023.

Naye Mkuu wa shule, Padri Wawelu ameipongeza Serikali kwa maboresho mbalimbali ya Elimu yenye kuleta tija nchini.

Katika mahafali hayo,TET imetoa zawadi ya vitabu vya kiada nakala 60 kwa shule ya Loyola zenye thamani ya shilingi 865,000 ambapo Mkurugenzi Mkuu amewaomba uongozi wa shule hiyo kuwapa nafasi wanafunzi wote kuweza kupata muda wa kusoma vitabu hivyo ambavyo vitawekwa kwenye maktaba za shule hiyo.

Mahafali hayo Wanafunzi 89 kati yao Wavulana 53 na Wasichana 36 ambalo ni ongezeko la wanafunzi 15 zaidi ya wahitimu wa mwaka jana,2022.

Wanafunzi hao wanafikisha jumla ya Wanafunzi 7,319 waliohitimu toka mahafali ya kwanza shuleni hapo mwaka 1999.
Shule hiyo ni miongoni mwa shule zaidi ya 845 duniani kote zinazoongozwa na Shirika la Yesu, Shirika la Mapadre wa Kanisa Katoliki (yaani Society of Jesus wanaojulikaja kama JESUITS).

Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dk.Aneth Komba akizungumza katika tukio hilo la wahitimu wa kidato cha Sita shule ya Sekondari ya Loyola ya Mabibo jijini Dar es Salaam mwaka 2023,

Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dk.Aneth Komba akikabidhi zawadi ya vitabu vya kiad kwa mkuu wa shule ya Loyola, Padri Martin Wawelu

Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dk.Aneth Komba ?katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu wa kidato cha Sita shule ya Sekondari ya Loyola ya Mabibo jijini Dar es Salaam mwaka 2023,


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...