Na Neema Mbuja, DODOMA


Mhe. Kassim Majaliwa ametembelea maonesho ya nishati

yanayoendelea jijini Dodoma na kuwataka wafanyakazi wa TANESCO kuendelea kuchapa kazi licha ya changamoto mbalimbali ili kupata mafanikio ya utendaji wao.


Mhe. Majaliwa ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na viongozi na watendaji wa taasisi mbalimbali zilizoko chini ya Wizara ya Nishati mara baada ya kutembelea maonesho yaNishati yanayoendelea kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma ambapo amesemaanaridhishwa na utekelezaji na maendeleo ya miradi ya kimkakati kama bwawa la kufua umemela mwalimu Nyerere unaotekelezwa na TANESCO ambapo mradi umefikia asilimia 86.89.


“Hatuna mashaka na utendaji wenu wa kazi na utaalamu wenu, endeleeni kuchapa kazi,

imarisheni utoaji wa huduma, lugha iwe nzuri kwa wateja tutafika tu” alisema Majaliwa

Akimkaribisha waziri mkuu,Mhe. January Makamba Waziri wa Nishati amesema kwa sasa

serikali kupitia wizara ya nishati inatoa kipaumbele kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikiakwa kushirikiana na ofisi ya makamu wa rais ili kuwahamisha wananchi kutumia nishatimbadala na kuhifadhi mazingira.


Katika hatua nyingine amepongeza watendaji wa TANESCO wanaofanya kazi kwenye maeneombalimbali na kuwataka kuendelea kuwa watoa huduma wazuri kwa wananchi bila kuchoka.


Baadhi ya wabunge waliotembelea kwenye mabanda ya TANESCO kwenye maonesho

yanayoendelea mjini Dodoma ni pamoja na Mhe. Anna Lupembe, Mhe. George simbachawene,Mhe. Prof. Paramagamba kabudi, Mhe. Hussein Bashe, Mhe. Hamis Mwinjuma ambapo kwanyakati tofauti wamesifu hatua iliyofikiwa kwenye utekelezaji wa mradi wa bwawa la kufuaumeme la Mwalimu Nyerere ambapo wamesema pindi utakapokamilika utaleta mapinduzimakubwa kwenye sekta ya umeme nchini.







 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...