Na Jane Edward, Arusha
Zaidi ya vijana Mia moja wanaosoma katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania wamenufaika na mpango wa ukuzaji Wanafunzi kitaaluma na kitaalam ambao unamwezesha kumjengea uwezo wa kujiajiri ama kuajiri mwenyewe akiwa bado chuoni.
Akizungumza jijini Arusha na Mkuu wa sehemu -Mpango wa ukuzaji wanafunzi kitaaluma na kitaalaam,Imani Matonya wakati akizungumza jijini Arusha.
Amesema kuwa,mpango huo ulianza mwaka jana na unawawezesha wanafunzi hao kupata ujuzi wa kutosha ambao unamwenzesha kwenda kujiajiri ama kuajiri wengine pindi anapohitimu chuo kwani wanaanza kujiajiri wakiwa tangu na vyuoni,hivyo wakihitimu wanakuwa na ujuzi huo tayari .
Ameongeza kuwa,kupitia mpango huo idadi kubwa ya wanafunzi wameweza kujiajiri kwa kuanzisha bunifu zao mbalimbali ambazo zimewawezesha kufanya maswala mbalimbali na hatimaye kupata ujuzi huo mapema wakiwa tangu vyuoni.
"Kwa kweli vijana hawa tumekuwa tukiwaandaa mapema sana kwa kuwajengea uwezo namna ya kujiajiri wanapokuwa vyuoni kwani changamoto kubwa inayowakabili wengi wao ni kuishia kukaa mtaani bila kuwa na shughuli zozote za kufanya hivyo kupitia bunifu zao Sisi tunawaunganisha na masoko kabisa. "amesema.
Aidh ameongeza kuwa ,kupitia idara ya ukuzaji maendeleo ya wanafunzi kitaaluma na kitaalam wanahakikisha wanafunzi wakitoka chuoni hapo wanaenda kufanyia kazi ujuzi wao waliounza na mawazo yao popote wanapokuwa na kuwa mabalozi wa kuwasaidia wengine.
Akibainisha baadhi ya changamoto zinazowakabili katika utekelezaji wa mpango huo ni swala la bajeti hususani kwa wanafunzi katika kutekeleza bunifu zao kwani wanafunzi wengi hawana vigezo vya kupata mikopo kutokana na kuwa wengi wao wanatoka mikoa mbalimbali hivyo kuwawia vigumu kupata mikopo hiyo.
Amesema kuwa,kutokana changamoto hiyo kuanzia mwakani wamejipanga kuhakikisha wanaanzia mfuko maalumu kwa ajili ya kusaidia wanafunzi wake kutekeleza maswala hayo.
Alitoa rai kwa vijana kuongeza bunifu zao kwa kutumi fursa mbalimbali zilizopo ili kuweza kuendeleza bunifu zao na kuweza kupata masoko katika maeneo mbalimbali.

Ezekiel Kasike mwanafunzi wa mwaka wa tatu (TIA)akionyesha bunifu ya utengenezaji wa diar aliyobuni mwenyewe pamoja na mifuko.
.jpeg)
.jpeg)
Wanafunzi wakisikiliza maelekezo ya shughuli zinazofanywa katika Chuo hicho!

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...