Benki ya Maendeleo TIB imekuwa mshindi wa Kwanza kwa upande wa Taasisi za Fedha zilizoshiriki Maonesho ya 10 ya Biashara na Utalii Tanga, yaliyokua yakifanyika katika Viwanja vya Mwahako Jijini Tanga.
Benki ya Maendeleo TIB ilifuatiwa na Benki ya NMB na Mfuko wa SELF (SELF Microfinance Fund). Pia, Benki ya Maendeleo TIB ilifanikiwa kushika nafasi ya tatu kwenye Taasisi za Bima/Bima-Benki zilizoshiriki maonesho hayo.
Maonesho ya 10 ya Biashara na Utalii Mkoa wa Tanga yalianza tarehe 28 Mei na kufikia tamati tarehe 6 Juni, 2023 yaliyokua na kauli mbiu: “Kilimo, Viwanda, Utalii na Madini ndio msingi wa maendeleo ya kiuchumi”.
Meneja Uhusiano na Masoko wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Saidi Mkabakuli (kulia) akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Waziri Kindamba alipotembelea Banda la Benki hiyo, katika Maonesho ya 10 ya Biashara na Utalii Tanga, yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwahako Jijini Tanga.
Meneja Uhusiano na Masoko wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Saidi Mkabakuli akitoa maelezo kuhusu benki kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Waziri Kindamba alipotembelea Banda la Benki hiyo.
Afisa Biashara na usimamizi wa Miradi wa Benki ya Maendeleo TIB Bi.Sonia Mlaki akizungumza na baadhi ya wananchi waliotembelea Banda la Benki hiyo wakati wa Maonesho ya 10 ya Biashara na Utalii Mkoa wa Tanga.
Wafanyakazi wa Benki ya Maendeleo TIB wakionesha Ngao ya Ushindi kwa
Upande wa Taasisi za Fedha zilizoshiriki Maonesho ya 10 ya Biashara na
Utalii Mkoa wa Tanga. Kutoka kushoto ni Bi Giusy Mbolile, Bw. Saidi
Mkabakuli (katikati) na Bw. Alex Mbambaga. Maonesho ya 10 ya Biashara na
Utalii Mkoa wa Tanga yalianza tarehe 28 Mei na kufikia tamati tarehe 6
Juni, 2023 yaliyokua na kauli mbiu: “Kilimo, Viwanda, Utalii na Madini
ndio msingi wa maendeleo ya kiuchumi”.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...