Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT)imeelezea hatua kwa hatua jinsi ambavyo mwenendo wa uchumi wa dunia umeathiri uchumi wetu na hasa upatikanaji wa fedha za kigeni hapa nchini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Juni 6,2023 wakati wa semina iliyoandaliwa na BoT kwa Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tafiti za Uchumi na Sera BoT Dkt. Suleiman Misango amefafanua mwenendo wa uchumi wa dunia umesababisha bei za bidhaa katika soko la dunia zipande na kupanda huko katika soko la dunia umesababisha mahitaji ya fedha za kigeni kuongezeka, hicho ni cha kwanza

Amesema baada ya kupanda kwa bei ya bidhaa katika soko la dunia wameona benki kuu nyingi hasa za nchi zilizoendelea zilichukua hatua za kupunguza ukwasi wa fedha zao katika chumi zao.Kwa mfano Benki Kuu ya Marekani imekuwa ikipunguza ukwasi kwa kiasi kikubwa sana.

"Sasa hii ikafanya riba katika masoko ya Marekani kuongezeka kwa hiyo riba ilipoongezeka kule unaona kwamba sasa fedha za mitaji ambazo zilikuwa zinaelekea kwenye nchi zinazoendelea kama Tanzania zikawa zimepungua zikaelekea kwenye soko la Marekani.Kwa maana hiyo kukawa kumesababisha uhaba wa fedha za kigeni hapa nchini.

"Tunatarajia kwasababu kuanzia kipindi cha Januari hadi hivi sasa tumeona hata utekelezaji kwa nchi zilizoendelea hususan Marekani imeanza kupungua kwa hiyo inaashiria kwa siku za baadae zile fedha ambazo zilikuwa zinaelekea Marekani zitaanza kuelekea kwenye nchi nyingine ikiwemo Tanzania.

"Lakini ni kwamba bei za bidhaa katika soko la dunia ambazo zilipanda kwa kiasi kikubwa sana hususan mafuta tumeona bei imekuwa ikishuka kuanzia Desemba na sasa hivi bei zimeshuka kwa kiasi kikubwa sana na kadri inavyoendelea kushuka ndio mahitaji ya fedha za kigeni yanakuwa yanapungua, " amesema.

Ameongeza pamoja na mabadiliko hayo ambayo wameanza kuona unafuu kwenye mwenendo wa uchumi wa dunia hapa nchini wao Benki Kuu na Serikali wamekuwa wakichukua hatua za kuhakikisha kwanza wanaongeza ukwasi lakini kuna hatua nyingine za kukabiliana na hali hiyo na nyingine kwa maana ya kuongeza ukwasi wa dola katika uchumi wetu.

Pia kuna hatua zingine ambazo wamezungumza hapa za kuhakikisha kwamba zinapunguza mahitaji ya fedha za kigeni kadri ya uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje .

Katika hiyo mikakati amesema maduka ya fedha wameongeza usajili na wataendelea kuongeza usajili kwasababu mwanzoni na walifanya utafiti wakagundua mojawapo ya vitu vilivyokuwa vinachangia kupunguza mzunguko wa fedha za kigeni hususan dola ya Marekani ilikuwa upatikanaji wa maduka ya kubadilishia fedha za kigeni

"Kama unavyofahamu maduka mengi ya fedha za kigeni ikifika muda wa saa 10 au saa 11 jioni yanatakiwa yawe yamefungwa kwa hiyo yule mtu aliyekuwa na fedha za kigeni anataka kubadilisha anakuwa hana nafasi ya kubadilisha.

" Kwa maana hiyo unakuwa umeshapunguza uwezekano wa hiyo fedha kuingia kwenye mzunguko, kwa hiyo tumeongeza maduka ya fedha za kigeni na mpaka sasa hivi Tanzania nzima kuna maduka ya kubadilishia fedha za kigeni 88 ambayo yamesambaa Tanzania Bara na Zanzibar na tutaendelea kuongeza kuhakikisha huduma hiyo inakuwa kwa urahisi zaidi, "amesema Dk.Misango.



Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tafiti za Uchumi BoT, Dkt. Suleiman Misango, akiwasilisha mada yake iliyohusu mapitio ya maendeleo ya uchumi nchini na fedha za kigeni wakati wa kikao kazi kati ya Benki Kuu ya Tanzania BoT na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kilichofanyika Juni 6,2023 katika ukumbi wa benki hiyo jijini Dar es Salaam.





Baadhi ya Picha mbalimbali zikiwaonesha baadhi ya wahariri wa Vyombo vya Habari pamoja na Wafanyakazi waandamizi wa BoT wakifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa kuhusu mwenendo wa uchumi na fedha za kigeni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...