Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV- Iringa
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi( CCM)Daniel Chongolo amesema uamuzi wa Serikali kujenga Uwanja wa Ndege Nduli mkoani Iringa umelenga kufungua fursa kwa wananchi wa Kusini.
Akizungumza leo Juni 1, 2023 baada ya kukagua upanuzi wa ujenzi wa Kiwanja cha Ndege Nduli Kilichopo Iringa,Katibu Mkuu Chongolo amesema uwanja huo unakwenda kufungua fursa za kiuchumi , hivyo ameshauri wananchi wa mkoa huo kuutumia.
"Wananchi wa Mkoa wa Iringa tumieni
vizuri uwanja wa Ndege wa Nduli uliopo mkoani hapa baada ya kukamilika na tumaamini uwanja huu unakwenda kuongeza uchumi wao pamoja na kusafirisha mazao."
Pia amesema utalii utakwenda kufungua mara baada ya kukamilika kwa uwanja huo wa Nduli , hivyo wananchi watapata fedha za kigeni na hayo ndio maendeleo ambayo Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inataka kuona yanatokea nchini.
Wakati huo huo Katibu Mkuu Chongolo ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi Mkoa wa Iringa kuendelea kutunza utamaduni wa mkoa huo ili wageni wanaoingia wajue utamaduni sambamba na kuwarithisha kizazi kijacho badala ya kuendelea kuiga mila za nchi nyingine.
Chongolo yuko mkoani Iringa akiwa ameongozana na Wajumbe wawili wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambao ni Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Haji Ussi Gavu na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,kwa ziara yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya Chama Cha Mapinduzi( CCM) ya mwaka 2020-2025 pamoja na kusikiliza kero za wananchi kwa lengo la kuzipatia ufumbuzi.
Katibu MKuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.Halima Dendego wakati akikagua upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Iringa
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akisikiliza maelezo kuhusu upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Iringa alipotembelea kujionea maendeleo ya Ujenzi wake ambapo hadi sasa Ujenzi umefikia zaidi ya asilimia 50.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...