



Na.Mwandishi Wetu-DODOMA
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).Dkt. James Andilile, leo 30 Mei 2023, ameshiriki kutoa elimu ya udhibiti wa huduma za nishati katika maonesho ya Wiki ya Nishati yanayoendelea katika viwanja vya Bunge, jijini Dodoma.
Dkt Andilile amewaelimisha wadau mbalimbali waliotembelea banda la EWURA kuhusu utaratibu wa kupata leseni za umeme, shughuli za petroli na gesi asilia pamoja na namna ya kuwasilisha malalamiko yanayohusu huduma zinazodhibitiwa; sanjari na namna EWURA ilivyorahisisha masharti ya leseni za vituo vya mafuta maeneo ya vijijini ili wananchi wa maeneo hayo wapate huduma hiyo kwa urahisi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...