Na Janeth Raphael - Michuzi Tv - Dodoma
Inakadiriwa kila mwaka Dunia inatumia mifuko bilioni 500 ya mifuko ya plastic na asilimia 10 ya taka zinazozalishwa zinatokana na plastic na sehemu kubwa takriban asilimia 80 ya taka zinazoishia baharini na katika maziwa kupitia kwenye mito, mitaro ya maji ya mvua na hata upepo ni taka za plastic.
Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango ameyabainisha hayo leo Jijini Dodoma katika kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani ambapo Kimataifa yamefanyika nchini Ivory Cost na Kitaifa yamefanyika Dodoma katika soko la machinga Jijini humo.
Makamu wa Rais Dkt Mpango amesema mwaka 2029 aliyekuwa Makamu wa Rais kwa kipindi hicho ambaye kwa sasa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Samia Suluhu Hassan alifanya kampeni ya kuongoza Serikali kufanya uamizi wa kusitisha matumizi ya mifuko ya plastic nchi nzima na kuagiza mifuko mbadala itumike ambayo ni rafiki kwa Mazingira ya wananchi.
"Kampeni hiyo Ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa na Tanzania ikaanza kusifika kuwa miongoni mwa nchi zinazofanikiwa kupunguza taka za plastic lakini kwa sasa inasikitisha tunaona matumizi ya mifuko hiyo imeanza kurudi tena kwa Kasi" Amesema Dkt Mpango.
Dkt mpango amesema taka za plastic zimeongezeka kwenye maeneo mengi ya wakazi, mifereji ya maji, kandokando ya barabara na maeneo ya wazi taka za plastic zimeongezeka, Nchini Tanzania inakadiriwa tani 350,000 ya mifuko ya plastic inazalishwa kila mwaka na zaidi ya asilimia 70 ya taka za bahari ya Hindi zinatokana na plastic na hali hii ikiendelea kuwepo wavuvi watakuwa wanavua plastic badala ya kuvua samaki.
"Mifuko ya plastic inachukua miaka 400 mpaka miaka 1,000 ndiyo ioze hivyo ni wazi haiwezekani hali hii iachwe iendelee" -Dkt Mpango
Kwa kuzingatia hali ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira ilivyo sasa bado kuna ukiukwaji wa sheria ambao unafanywa na baadhi ya wafanyabiashara wanaozalisha au kuingiza mifuko ya plastic kinyemela kutoka nje na wafanyabiashara sokoni wanaotumia mifuko hiyo kama vibebeo au vifungashio vya bidhaa na kuridhisha nyuma hatua ambayo ilishafikiwa na nchi.
Aidha Dkt Mpango amewataka watanzania wote kuhakikisha kazi ya kudhibiti taka za plastic inaendelezwa na ni lazima jambo hilo lifanikiwe na kuendelea kupiga vita matumizi ya bidhaa za mifuko ya plastic na kuimarisha utunzaji wa mazingira hasa baharini, maziwa, mito na mifereji ili kuepuka uchafuzi ambao unatokana na taka hizo za plastic.
Hata hivyo Dkt Mpango ametoa maelezo kwa Baraza la Taifa la hifadhi na usimamizi WA Mazingira (NEMC) pamoja na mamlaka za Serikali za mitaa nchi nzima kusimamia na kuongeza nguvu katika utekelezaji wa katazo la matumizi ya bidhaa za mifuko ya plastic
" Hakikisheni mnachukua hatua za kisheria kwa wale wanaokiuka maagizo haya" - Dkt Mpango.
Awali Waziri wa Nchi Ofisi ya Raise Muungano na Mazingira Dkt Selemani Jafo akimkaribisha mgeni Rasmi amesema sherehe za mwaka huu zimekuwa tofauti badala ya kwenda kufanya sherehe hizo katika ukumbi ajenda ya mazingira wameamua mwaka huu kwenda kushugulika na wananchi mitaani na kutoa hamasa kwa wananchi hao kujenga tabia ya kufanya usafi katika mazingira yao mara kwa mara na sio kusubiri siku ya Mazingira tu.
Dkt Jafo amemuhakikishia Makamu wa Rais Dkt Mpango kuwa agenda ya Mazingira iko salama na kazi inaenda vizuri site.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya kudumu ya maji na mazingira Jackson Kiswaga amesema mazingira ni uhai wa kila Mtanzania hivyo kuna wajibu mkubwa wa kutunza mazingira na kuwa chachu kuhimizana na kutoa elimu kwa kila mtu anayekuzunguka katika eneo lako na baadae kubadilika kuwa tabia ya kutunza mazingira na yabaki salama yakiwa masafi.
Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Muungano na Mazingira Dkt Seleman Jafo wakiwa sehemu ya waliofanya usafi katika soko la machinga leo juni 5, 2023 jijini Dodoma ikiwa ni maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...