Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
JENGO la Hifadhi House jijini Dar es Salaaam limenusurika kuwaka moto baada ya eneo la juu katika jengo hilo kuzuka moto.
Kabla ya moto kuanza kuwaka leo Juni 30, 2023, ulionekana moshi mzito katika kingo ya jengo hilo iliyopo katika ghorofa ya tisa, moshi huo mzito ulisababisha watu waliokuwa karibu na jengo hilo kuanza kuulizana maswali kama ni jengo linaungua au laa.
Hata hivyo kadri moshi ulivyokuwa ukiendelea baadae kidogo moshi huo ukawa umeambatana na moto, hali iliyoongeza taharuki kwa waliokuwa wanaangalia jengo hilo
Kutokana na moto kuonekana kushika kasi mmoja ya wananchi waliokuwa eneo hilo aliyejitambulika kwa jina la Abeid Dims Zumbe aliamua kwenda kutoa taarifa kwa askari waliokuwa eneo la mapokezi.
"Wakati tunaendelea kushangaa na kuulizana, wengine walishauri tukatoe taarifa hivyo nikaenda kwa walinzi wa jengo na kuwaambia, wakati huo hawakuwa na taarifa yoyote, niliwaambia juu ya jengo kuna moshi unatoka lakini pia tunaona moto nao umeanza kuwaka, nendeni mkaangalie na kisha muwaambie watu wa zima moto, " amesema Zumbe.
Hata hivyo baadhi ya watu waliokuwa kwenye jengo hilo baada ya kupata taarifa walikwenda juu ya jengo hilo na kuanza kuzima moto huo na hivyo kunusuru jengo hilo kuwaka.
Wakati waliokuwa kwenye jengo hilo kufanikiwa kuzima moto huo gari ya Jeshi la Zima Moto na Uokoaji walifika kwenye jengo hilo kwa ajili ya kujiridhisha iwapo moto umezima au laa Gari ya Zima moto ilifika kwenye jengo hilo saa 8.40 ikiwa ni dakika 40 ya baada ya kuonekana moto huo.
Hata hivyo Michuzi TV na Michuzi Blog iliyokuwa ikishuhudia moshi na baadae moto huo, ilizungumza na baadhi ya watu wenye ofisi kwenye eneo hilo ambao hawakuwa tayari kuzungumza chochote kwa madai wapo wanaohusika na jengo hilo na ndio wanaweza kuelezea kilichotokea.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...