KAMPUNI Ya Uzalishaji wa mbolea Afrika (OCP) yazindua rasmi awamu ya tatu ya Mradi wa tathmini ya udongo ili kutoa elimu kwa wakulima juu ya aina za udongo na mazao rafiki kulimwa katika mikoa husika.

Mkurugenzi wa Kampuni ya OCP Hillary Pato ameyasema hayo leo Juni 30, 2023 wakati akizindua Mradi huo amesema OCP ikishirikiana na Serikali imeandaa mchakato wa upimaji wa udongo zaidi ya vijiji 100 ndani ya Mkoa wa Musoma lengo likiwa ni kuelimisha wakulima kuhusu udongo wa eneo lao bila ya gharama zozote kwa wakulima hao.

"Mradi huu wanufaika watakuwa wakulima zaidi ya vijiji 100 ndani ya Mkoa wa Mara ambapo kupitia mpango huo wa upimaji udongo ulioandaliwa na Serikali juu ya kutoa elimu kwa wakulima nini kifanyike ili kutunza ubora wa udongo ambapo kila kijiji zaidi ya wakulima 100 watafikiwa," amesema.

Ameongeza kwamba mradi huo wa upimaji na tathmini ya udongo unatarajiwa kuendeshwa katika vijiji 400 na kuwafikia wakulima wapatao 40,000 kufikia mwisho wa 2023.

Amefafanua mradi huo tayari umewanufaisha wakulima 39,0000 katika nchi nane katika Bara la Afrika ikiwemo Nigeria, Togo, Ghana, Kenya,Burkina Faso,cote D'Ivoire na Senegal pamoja na nchi ya Tanzania kuwa moja wa nchi wanufaika wa mradi huo.

Ametoa mwito kwa wakulima kuhakikisha wanakuwa na teknolojia za kisasa zitazowawezesha kuongeza uzalishaji wao na hivyo kuondokana na umasikini. "Mradi huu wa upimaji na tathmini ya udongo ni jambo la kipekee sana na hivyo tunahamasisha wakulima wote wawe sehemu ya mradi huu."

Kwa Upande wake Mwanasayansi wa udongo kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) Fredrick Mbowe ameongeza kuwa Mradi wa Upimaji na tathmini wa udongo unaoongozwa na OCP kwa sasa ni nyenzo madhubuti kwa wakulima utakaokua na msaada mkubwa kwa kuongeza kiwango cha uzalishaji mazao.

Ameeleza taasisi hiyo ya tari iliundwa kutatua changamoto za upimaji wa udongo,Sampuli pamoja na kutoa nasaha zitakazo imarisha ukuaji kilimo katika ngazi za Vijiji,Wilaya, na Mkoa kwa kushirikiana na Kampuni ya OCP Afrika na Serikali za mitaa.
Mkuu wa Idara ya Udongo na Mtafiti Mkuu kutoka taasisi ya utafiti wa kilimo (TARI) Ndg. Fredrick Mlowe akitoa wasilisho juu ya hali ya rotuba katika Mkoa kwenye uzinduzi rasmi wa awamu ya tatu ya mradi wa Utafiti na Upimaji wa afya Udongo (OCP School Lab) wilayani Musoma mkoani Mara.

Mkurugenzi taasisi ya utafiti wa kilimo (TARI) Dkt. Dennis Tippe akitoa taarifa fupi juu ya manufaa ya utekelezaji wa mradi wa Utafiti na Upimaji wa afya Udongo (OCP School Lab) wakati wa Uzinduzi rasmi wa awamu ya tatu ya mradi huo wilayani Musoma mkoani Mara.

Meneja ya mamlaka ya udhibiti wa Mbolea (TFRA) kanda ya ziwa Dkt. Asheri Kalala akitoa wasilisho juu ya hali ya uzalishaji na upatikanaji wa pembejeo wakati wa Uzinduzi rasmi wa awamu ya tatu ya mradi wa Utafiti na Upimaji wa afya Udongo (OCP School Lab) wilaya ya Musoma mkoani Mara.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...