Na Damian Kunambi, Njombe
Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) Nicolaus Shombe amesema kwamujibu wa tafiti iliyofanyika mwaka 2013 iligundua kuwa miradi ya Liganga na Mchuchuma itachimbwa kwa miaka mingi ambapo kwa upande wa Mchuchuma ambako kuna mradi wa makaa ya mawe wenye Tani Ml. 428 kwenye eneo la km za mraba 30 yanatarajiwa kuchibwa kwa miaka zaidi ya 140 huku chuma cha Liganga kikiwa na ukubwa wa zaidi ya Tani Ml. 126 ambazo zitachimbwa kwa miaka isiyopungua 56.
Hayo ameyasema katika hafla ya uzinduzi wa ulipaji fidia kwa wananchi wanaopisha miradi hiyo ambapo hafla hiyo imehudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali, wabunge wa mkoa wa Njombe akiwemo mbunge wa Ludewa Joseph Kamonga pamoja na wananchi wanaoenda kulipwa fidia huku mgeni rasmi akiwa ni Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Ashatu Kijaji.
Amesema kwa sasa wameshaanza zoezi la ulipaji fidia kwa wananchi zaidi ya 1000 ambapo kiasi cha Sh. Bl. 15.4 zitaenda kulipa wananchi hao na tayari baadhi yao wameshaanza kuingiziwa fedha hizo huku wengine wakiendelea kuingiziwa fedha hizo.
"Tayari watu 39 wamekwisha ingiziwa malipo yao kwenye akaunti na bado tunaendelea kuingizia wengine hivyo tunatarajia ndani ya siku tano tutakuwa tumekamilisha malipo haya kwa kila mnufaika"
Aidha kwa upande wake Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Ashatu Kijaji amesema miradi hiyo imekuwa ikiandikwa kwenye vitabu na kuwepo kwenye dira ya Taifa ya miaka 25 ambapo tangu mwaka 2000 uliandikwa uanze kutekelezwa.
Amesema miradi hiyo itakapokamilika utaokoa fedha nyingi za kigeni zaidi ya dola Bl. 1 ambazo zimekuwa zikitumika kwa mwaka mzima katika uagizaji wa bidhaa za chuma hivyo badala ya kuendelea kupoteza fedha hizo zitaelekezwa katika huduma nyingine za kijamii.
"Taifa lipo katika hali ngumu kwa sasa ya upatikanaji wa dola za kimarekani lakini sisi tunatumia dola za kimarekani zaidi ya Bl. 1 kwa mwaka kqa kuagiza chuma ambacho tayari tunacho imefika wakati sasa watumishi wenzangu ndani ya wizara na NDC tuseme basi inatosha hakuna muda tena wa kusubiri na majadiliano yasiyo na kikomo", alisema Dkt. Kijaji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...