MHASIBU wa Jiji la Dar es Salaam, Alinanuswe Mwasasumbe (60) amefikishwa Mahakaka ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na tuhuma za kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka 13, limo la utakatishaji na kuisabishia Halmashauri hasara ya Sh. bilioni 8.9
Mshtakiwa Mwasasumbe anayeishi Mbagala Maji Matitu jijini Dar es Salaam amesomewa mashtaka yake mbele ya Wakili wa Serikali Mwandamizi Fatuma Waziri akishirikiana na Veronica Chimwanda.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Ferdinand Kihwonde imedaiwa, kati ya Julai Mosi 2019 na Juni 30, 2021 katika ofisi za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa mtumishi wa umma kwa nafasi ya Mhasibu, alitumia madaraka yake vibaya kwa kushindwa kuweka kiasi cha Sh. 8.9 kwenye akaunti za Jiji hilo zilizopo katika benki ya NMB, CRDB, NBC, DCB.
Inadaiwa kiasi hicho cha fedha ni mapato yaliyokusanywa kutoka katika vyanzo mbalimbali vya mapato ya Jiji hilo na hivyo kujipatia manufaa yasiyofaa kiasi ya kiasi hicho cha fedha.
Katika shtaka la kughushi, mshtakiwa anadaiwa Februari 28, 2021 katika ofisi hizo, kwa nia ya kudanganya, alitengeneza nyaraka ya uongo yenye kichwa cha habari 'Kurudishwa fedha iliyotumika kuanzia Februari Mosi hadi February 28, 2021' akionyesha kiasi cha Sh. Milioni 5.9 kimerudishwa kama kilivyoombwa ili kitumike kuwalipa vibarua na matumizi mengine, wakati akijua kuwa si kweli.
Aidha mshtakiwa anadaiwa katika kipindi hicho hicho, alijipatia Sh. Bilioni 8.9 kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, wakati akijua kuwa fedha hizo ni zao la kosa tangulizi la kughushi.
Pia, mshtakiwa anadaiwa kati ya Julai Mosi 2019 na Juni 6, 2021 kwa makusudi na huku akiwa nia ya kutenda kosa huku alisababishia hasara ya Sh. 8.931, 589,500 kwa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam huku akijua kufanya hivyo ni kinyume cha Sheria.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 10, 2023 itakapotajwa.Mshtakiwa amerudishwa rumande.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...