Na Karama Kenyunko Michuzi TV

ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Samwel Kamanga na wenzake sita wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na jumla ya mashtaka 365 likiwemo shtaka la kuongoza genge la uharifu na kujipatia zaidi ya sh. bilioni moja mali ya NIC.

Mashtaka mengine mbali na kuongoza genge la uhalifu ni kughushi, kutoa nyaraka za uongo, kuchepusha fedha na utakatishaji wa fedha na kulisababishia Shirika hilo hasara.

Hata hivyo, mahakama imewasomea washtakiwa hao mashtaka 101 tu kabla ya kesi hiyo kuahirishwa hadi Juni 6, 2023.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na Wakili wa Serikali kutoka Takukuru Ipyana Mwakatobe akisaidiana na Wakili wa Serikali Mwandamizi Grace Mwanga imewataja washtakiwa wengine mbali na Kamanga ni, Kaimu Mhasibu Mkuu wa zamani wa NIC, Tabu Kingu, wahasibu Victor Mleleu, Peter Nzunda, Kenan Mpalanguro, Lisubilo Sambo na Mfworo Ngereja.

Katika shtaka la kuongoza genge la uhalifu imedaiwa Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Evodia Kyaruzi kuwa, washtakiwa walitenda kosa hilo kati ya Januari Mosi 2013 na Desemba 31, 2018 katika maeneo tofauti tofauti jijini Dar es Salaam, mkoani Rukwa, Kilimanjaro, Arusha, Mbeya, Morogoro na Kigoma.

Inadaiwa katika kipindi hicho washtakiwa kwa makusudi waliongoza genge la uhalifu ili kujipatia sh. 1,863,017,400.76 kwa njia ya ulaghai kutoka Shirika la Taifa la bima.

Kesi hiyo itaendelea Jumatatu, Juni 5, 2023 watuhumiwa wamerudishwa mahabusu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...