-Wananchi wafurahia kusogezewa kituo karibu na makazi yao, waishukuru Serikali
Na Said Mwishehe, Michuzi TV –Ukerewe
WAKALA
wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) kupitia Shamba la Miti Rubya lililopo
wilayani Ukerewe mkoani Mwanza wamekamilisha ujenzi wa kituo cha polisi
Serema ambacjo kimegharimu Sh.milioni 54 hadi kukamilika kwake.
Ujenzi
wa kituo hicho unatokana na uchakavu wa kituo cha polisi ambacho
kimekuwepo katika shamba la Rubya kwa muda mrefu, hivyo TFS iliona iko
haja ya kutoa fedha kujenga kituo cha polisi kipya, lengo likiwa
kuimarisha usalama wa msitu pamoja na mali za wananchi wanaozunguka
shamba hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari PCO Mhifadhi Mkuu
Shamba la Miti Rubya Festo Chaula amesema Shamba hili ni miongoni mwa
mashamba yanayosimamiwa na TFS na kati ya mwaka 1986 mpaka mwaka 2004
kulitokea wimbi kubwa la uhalifu mkubwa wa rasilimali zitokanazo na
misitu.
“Hivyo Serikali iliamua kuleta kituo cha polisi eneo hili
ili kukabiliana na uhalifu, hata hivyo hakukua na jengo ,kwa hiyo
shamba la miti Rubya liliamua kutoa jengo lake kwa niaba ya Serikali
ili kuwe na kituo hicho cha polisi.
“Hata hivyo kituo hicho
kimekuwepo kwa muda mrefu na kusababisha majengo yake kuwa chakavu
,kutokana na uchakavu wa kituo hicho ,shamba la miti Rubya kupitia TFS
kwa niaba ya Serikali tuliamua kukiboreha,”amesema PCO Chaula .
Aidha
amesema ilipofika nwaka wa fedha wa 2021/2022 Serikali kupitia shamba
la miti Rubya ilitoa Sh.milioni 54 kujenga kituo kipya polisi ambacho
kimejengwa eneo la Serema kwasababu pale kilipokuwepo awali lilionekana
ni eneo la hifadhi ya barabara lakini pia ni eneo la linalohistahili
kuachwa kwasababu za uhifadhi wa mazingira.
“Faifa ya kituo hiki
kitasaidia wananchi kupunguza uhalifu hasa kwenye shamba lenyewe pamoja
na wannchi wote wanaozunguka hili shamba,”amesema na kuongeza mbali ya
kujenga kituo hicho wamekuwa wakisaidia katika kufanikisha miradi
mbalimbali ya maendeleo.
Amesema shamba la miti Rubya pia
lilishajenga Zahanati ambayo inahudumia wananchi wanaozunguka shamba
hilo huku akifafanua pia wamesaidia ujenzi wa madarasa,wametoa bati 96
kwa ajili ya Shule ya Msingi Rubya pamoja na mifuko ya saruji 100 katika
kijiji cha Serema.
“Kazi za uhifadhi zinaendelea kama kawaida
lakini pia kituo hiki kuwepo hapa jirani tunapata usalama mkubwa na hata
wananchi wanafurahi kwa kuamini watakuwa salama zaidi kwasababu kipo
karibu,”amesisitiza .
Kwa upande Mkaguzi Msaidizi wa Polisi na
Mkuu wa Kituo cha Polisi Rubya amesema wanaishukuru Serikali kupitia
TFS kwa ujenzi wa kituo kipya cha polisi Rubya na baada kukamilika kwa
kituo hicho matumaini yao wananchi watapa huduma karibu na makazi yao.
“Kwa
kituo hiki cha Rubya tunakwenda kuhudumia kata zima ya Bwiro yenye
vijiji vinne lakini pia baadhi ya vijiji vya Kata ya Mriti na kata ya
Igala, kwa hiyo tunatoa huduma kwa kata tatu.Kituo cha polisi Rubya
kimekuwa ni msaada muhimu katika kukabiliana na wahalifu na kwa sasa
hali ni nzuri sana,”amesema huku akisisitiza wamekuwa na ushirikiano
mkubwa na TFS pamoja na vijiji vyote vinavyozunguka msitu.
Wakati
huo huo Mtendaji wa kijiji cha Rubya Justinian Emmanuel ametumia nafasi
hiyo kutoa shukrani kwa TFS kwa kushirikiana na Serikali ya Kijiji kwa
kujenga kituo hicho ambacho tayari kimekamilika.
“Kwa kipekee
tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa msaada wa ujenzi wa kituo hiki
kwani kule kilipokuwepo awali tulikuwa tunatumia gharama kubwa kwenda
kufuata huduma , sasa huduma imesogea karibu kabisa na
wananchi,”amesema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya
Kijiji Serema Mkama Mjaya Mkama ametoa shukrani kwa shamba la miti Rubya
kwa kutoa ushirikiano na kujenga kituo hicho.
“Shamba la miti
Rubya walituandikia barua ya kuomba ardhi kwa ajili ya kujenga kituo cha
polisi, Serikali ya kijiji tuliona tunao uhitaji wa kuwa na kituo cha
polisi hivyo tulikubali kwa kutoa ardhi bila malipo yoyote,”amesema.
Mmoja ya wakazi wanaozunguka shamba hilo akikaokota kuni baada ya uongozi wa shamba hilo kuruhusu wananchi kuokota kuni
Muonekano wa jengo la zamani la kituo cha Polisi ambacho kilikuwa kinatumiwa kwa ajili ya kulinda usalama wa wananchi wanaozunguka shamba la miti Rubya .Kutokana na kuchaa kwa kituo hicho shamba hilo kwa niaba ya Serikali wamejenga kituo kipya cha Polisi Serema
Mhifadhi Mkuu wa Shamba la Miti Rubya wilayani Ukerewe mkoani Mwanza PCO Festo Chaula( wa tatu kutoka kushoto waliosimama mbele) akiwa na baadhi ya viongozi pamoja na wananchi wa Kijiji cha Serema ambako kimejengwa kituo kipya cha polisi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...