MWENYEKITI wa Vijana wa Chama Cha Tanzania Labour Party (TLP), Mhandisi Aivan Maganza amesema uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti chama hicho ngazi ya taifa utafanyika Juni 18, 2023.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini katika Makao Makuu ya TLP Magomeni jijini Dar es Salaam Mei 29,2023 Mhandisi, Maganza amesema kuwa hayo nimakubaliano yaliyofikiwa na Halmashauri kuu ya Chama hicho.
"Viongozi wote wa Makao Makuu, ambao namanisha wa Vitengo vya vijana, akina mama pamoja na wazee na mkutano mkuu Halmashauri kuu katika adhimio lake la Machi 05, 2023, tulikubaliana kwamba uchaguzi Mkuu TLP nafasi ya Mwenyekiti utafanyika Juni 18 Mwaka huu."
Amesema pamoja na uchaguzi huo kutakuwa na mkutano mkuu wa mwaka wa chama hicho pamoja na mambo mengine baadhi ya viongozi wa juu wa TLP walipiga saini za kutaka mkutano mkuu ufanyike.
“Tumekubaliana kwa pamoja mkutano mkuu wa TLP taifa wa kumchagua Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party utafanyika Juni 18, 2023, hivyo taarifa iwafikie wajumbe wa mkutano mkuu TLP taifa popote walipo kwamba chama makao makuu kwa kushirikiana na idara tutaandaa utaratibu wote, na tayari maandalizi yapo tayari kwamba tutakutana kwaajili ya uchaguzi.
Pia Mhandisi Maganza amewajulisha wagombea wote wajiandae kwaajili ya uchaguzi huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...