Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amesema kutokana na uhaba wa Ardhi katika Mkoa huo ujenzi wa vyumba vya madarasa ni vema kujenga madarasa ya ghorofa ili kutumia vizuri Ardhi iliyoko sasa watu wanaongezeka lakini Ardhi ni ileile.

RC Chalamila amesema hayo leo Juni 28,2023 katika muendelezo wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo Mkoa wa Dar es Salaam ambapo leo alikuwa katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

Mhe Chalamila amekagua ujenzi wa madarasa 20 ya Ghorofa na matundu ya vyoo 45 shule ya Sekondari Liwiti awamu ya kwanza na Jengo la pili ambalo ni Ghorofa madarasa 20 awamu ya pili katika shule hiyo.

Aidha amekagua ujenzi wa shule mpya yenye mikondo miwili (2) madarasa 14 matundu ya vyoo 18, kichomea taka na madarasa 2 ya awali pia matundu 6 ya vyoo Shule ya msingi kivule.

Hata hivyo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa juhudi kubwa katika kuboresha miundo mbinu ya elimu katika Jiji hilo na kuwataka makandarasi walioaminiwa kujenga majengo hayo kukamilisha kwa wakati na kuzingatia thamani ya fedha.

Mwisho Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Edward mpogolo amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kuyafanyia kazi maelekezo yake na kuendelea kusimamia vizuri miradi ya maendeleo katika Wilaya hiyo kwa masilahi mapana ya wana Ilala na Taifa kwa Ujumla





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...