Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
Mkuu
wa mkoa wa Pwani , alhaj Abubakari Kunenge, amepokea Ng'ombe 500 na
mbuzi 1,000 kutoka Jumuiya ya IDDEF ya nchini Uturuki wakishirikiana na
Rahma Fondation ya Tanzania kwa ajili ya sadaka ya sikukuu ya Eid Al
Adha .
Akikabidhi Sadaka
hiyo ,Sheh Bahadhir kutoka katika taasisi hiyo, katika machinjio ya
Pangani, mjini Kibaha, alisema IDDEF , taasisi ya Rahmah ya nchini
Tanzania wametoa ng'ombe na mbuzi hao kwa ajili ya Sadaka hiyo hususan
kwa wajane,yatima na wazee.
Aidha aliishukuru serikali ya Tanzania kwa kukubali msaada huo na kutoa machinjio hiyo kwa ajili ya kuchinjia wanyama hao.
Akipokea
msaada huo, Mkuu wa Mkoa Kunenge, aliishukuru taasisi hizo kwa sadaka
hiyo ya ibada ya kuchinjwa ya Eid Al adha na kwamba sadaka hiyo
itagawanywa kwa wahitaji ikiwemo, yatima,wajane na wazee.
"Nimepokea
Ng'ombe 500 na mbuzi 1,000 Kwa ajili ya sadaka ya ibada ya kuchinjwa ya
EId Al Adha naipongeza Jumuiya hii Rahma Foundation na IDDER na
mashekh wote kutoka Uturuki kwa kuendelea kushirikiana na nchi yetu
katika nyanja mbalimbali"alisema Kunenge.
Licha
ya hayo Kunenge alieleza ni vema Sadaka hizo zikatolewa Kwa wahitaji
ikiwemo yatima,wajane, wazee, watu wasiojiweza na waalimu wa dini.
Kwa
upande wake mwakilishi wa Shekh wa Mkoa wa Pwani, Salimini
Buda,aliishukuru taasisi hiyo na kwamba Sadaka hiyo itawafikia walengwa
kama ilivyokusudiwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...