Mkuu wa mkoa wa Arusha Arusha,John Mongela amewataka viongozi wa vyama vya ushirika mkoani humo kuacha tabia ya kuanzisha migogoro kwa lengo la kujinufaisha kwa masilahi yao binasfisi hali ambayo inapelekea kuharibu taswira ya vyama hivyo katika jamii.

Akizungumza katika jukwaa la maendeleo ya ushirika mkoa wa Arusha ,Mongela alisema kuwa kumekuwepo na baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika wamekuwa wanaanzisha migogoro makusudi kwa lengo lao la kujipatia maslahi yao binafsi.

"Unakuta kiongozi wa chama anatafuta namna ya kuhujumu ushirika , anafanya jambo la kichama kwa mlengo wake bila kushirikisha wanachama jambo ambalo linaleta migogoro na wanachama hali hii sio taswira nzuri,"alisema Mongela.

Aidha aliwataka viongozi wa ushirika wafanye kazi ya kuamasisha wananchi kuunda vyama vya ushirika ili vyama viwe vingi zaidi huku akibainisha kuwa ndani ya vyama hivyo kuna fursa nyingi zaidi ambazo zitawainua kiuchumi.

Mongela alisema ndani ya ushirika taasisi za kibenki zipo tayari kushirikiana nao na kwa wale wakulima serikali imerahisisha ata riba zimeshushwa na kuna fedha nyingi ambayo wapo wengi haijawafikia na itakuwa na tija nyingi na fedha hiyo sio kwa ajili ya kilimo cha shambani tu bali inawahusu hata wale ambao wanaongeza dhamani mazao .

kwa upande wake mwenyekiti wa jukwaa la maendeleo ya ushirika mkoa wa Arusha Wilibald Ngambeki alisema kuwa katika vyama vyao vya ushirika wanakabiliwa na tatizo la Tehama kwa kwa upande wa mijini inarahisisha kazi lakini kwa upande wa vijijini ni kikwazo kwa maendeleo ya ushirika kwani baadhi ya maeneo ya vijijini hayana huduma za intanet na kama ipo ni yaubora wa chini

Aliomba serikali kupitia mammlaka ya mapato Tanzania kuacha kulazimisha matumizi ya Tehama kwenye ku-file returns kwa walipakodi wote na badala yake wakubali matumizi ya njia zote ikiwemo ile ya zamani yakupeleka makaratasi hasa kwa vyama vilivyopo vijijini pamoja na kwamba yapo maboresho yanayoendelea kwenye mfumo wa kujaza ritani za kodi bado mfumo huo unachangamoto kwa watumiaji.

Alisema kuwa vyama vya ushirika vilivyovingi na hasa vya kijamii vinaanza kama kikundi vya kusaidiana inapofika hatua uamuzi ukafanywa wa kuanzisha chama chama ushirika inahama na ile miamala ya nyuma bahati mbaya vikundi hivi havina uelewa wa maswala ya kodi hivyo kujikuta na adhabu zinazotokana na kushidwa kufuata taratibu za kodi kitokana na hilo waliomba vyama vya ushirika kupewa likizo ya hadi miaka 10 kabla ya kufuata za kikodi ili kiwezesha chama kujenga uwezo wa ndani ikiwemo uwezo wa kuajiri wataalam.

Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela akimkabidhi funguo wa gari  na gari mrajis wa vyama vya ushirika mkoa wa Arusha Grace Masambaji  Kwa ajili ya kutumia kwa shughuli za chama hicho mkoani hapo gari hilo lilitolewa na mdau wa ushirika ambao shirika la Heirfer

 Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongele akiongea katika mkutano wa  jukwaa la maendeleo ya ushirika mkoa wa Arusha  lililofanyika  Jana (Leo)katika ukumbi wa club D uliopo ndani ya halmashauri ya jiji la Arusha (Pamela Mollel,Arusha)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...