Na Said Mwishehe, Michuzi TV
WATU 1000 katika Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na mikoa mingine tisa nchini Tanzania wameshiriki Siku ya kimataifa ya Yoga ambayo huambatana na mazoezi ya mwili pamoja na kufanya tafakari.
Kwa Dar es Salaam Siku ya Yoga ambayo kwa hapa nchini huandaliwa na Ubalozi wa India ambapo ndipo mchezo huo Yoga imefanyika katika Viwanja vya Gymkhana huku Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Said Yakub ameongoza washiriki katika siku hiyo.
Akizungumza leo kwenye maadhimisho hayo Katibu Mkuu Said Yakub amesema huu ni mwaka wa tisa sasa tangu Umoja wa Mataifa ulipotambua Yoga kama siku maalum yaani Juni 21 ndio hasa siku ambayo umoja huo umeitambua kwamba Yoga nayo itengewe siku yake.
"Kwa hiyo Ubalozi wa India umeandaa sherehe hizi ambazo zimehudhuriwa na zaidi ya watu 1000 wengi wakiwa wanatoka India lakini kwa hapa Tanzania sherehe hizi zimeazimishwa katika mikoa ya Tanga,Dodoma,Mwanza ,Arusha, Zanzibar ,Morogoro na Kilimanjaro.
" Kwa jumla takribani mikoa tisa imeshiriki na sisi kama Serikali tulipokea mualiko wa kushiriki katika eneo hili, lakini leo hii tulikuwa na watu kutoka Umoja wa Mataifa na Yoga inatambuliwa hivi sasa pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO) ambao Wana App maalum kwenye Website yao ambayo inaitwa Yoga App ,
"Kikweli hasa kama mlivyoona mazoezi ya Yoga yanahusisha vitu viwili , yanahusisha Kwanza mazoezi ya viungo ,mwili lakini yanahusisha fikra, unapewa muda wa kufanya tafakuri ukiwa na jambo lako gumu linakusumbua unasema lazima ufanye mazoezi hayo ya tafakuri.
" Ukae kimya peke yako katika eneo la wazi na unapata na upepo kidogo na kisha fikra zitakuja mpaka utapata suluhisho, kwa hicho ndicho kukibwa tumekifanya hapa leo,yamekuwa mazoezi mazuri sana ,yamehudhuriwa na watu wengi,"amesema.
Ameeleza kuwa amezungumza na baadhi ya washiriki wanasema wametoka katika maeneo mbalimbali kama Bagamoyo lakini pia wako watu wa umri mbalimbali kama ilivyotangazwa."Kijana mdogo kabisa kushiriki katika siku ya leo ana miaka mitatu lakini kulikuwa na mtu mzima mwenye miaka 85."
Ameongeza kwa hiyo watu wa umri mbalimbali,makabila na Mataifa mbalimbali na kimsingi Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo wanaunga mkono sherehe kama hizo za kitamaduni kutoka nchi mbalimbali kwasababu zinasaidia katika kutujenga kuwa wamoja
Ametoa ujumbe kwa Watanzani kujenga utamaduni wa kutenga muda kwa ajili ya kufanya mazoezi kwani yanasaidia katika kuujenga mwili na kukuepusha na magonjwa kama Kisukari, Shinikizo la damu na uzito uliopitiliza.
"Mazoezi kama haya ya Yoga kama mlivyoona leo kuna kujikunja kunja mwili ni mazoezi kamili ya mwili ambayo yanasaidia sasa katika kuufanya mwili kuwa imara na unapokuwa imara unaepukana na magonjwa.
" Kwa hiyo mwito wangu kwa Watanzania wangetenge muda wa katika siku ,nimesoma mahala ukifanya mazoezi kwa muda wa saa moja basi utakuwa umeongeza saa tatu za kuishi, kwa hiyo tujitahidi tutenge muda tufanye mazoezi.
"Lakini mazoezi mengine ambayo tumeyafanya hapa kwa muda mrefu ni ya fikra,hivyo ni vema upate muda mrefu utafakari ulikotoka, ulipo na unakokwenda na uwe peke yako katika eneo la wazi Tanzania ina hewa nzuri.Kwa wakazi wa Dar es Salaam wanaufukwe ambao hauko mbali, hivyo watenge muda wa kufanya tafakari na kujenga afya ya akili.
Kwa upande wake Balozi wa India nchini Tanzania Binaya S. Pradhan ametumia nafasi hiyo kuwashukuru wote walioshiriki kuadhimisha siku ya Yoga wakiwemo wanadiplomasia na wadhamini.
Amefafanua mwaka mwaka 2014 katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa uliitisha azimio ambalo lilipitishwa na nchi 177 Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi hizo kama mdhamini mwenza wa kumbukumbu ya siku ya Yoga Kimataifa kila mwaka.
"Watu kutoka kila tabaka hapa Dar es Salaam wamekuwa wakishiriki kikamilifu katika kusherehekea siku ya Kimataifa ya Yoga kwa miaka iliyopita. Siku ya Yoga Kitaifa huadhmishwa kila mwaka mwezi wa sita tarehe 21. Kila mwaka, Siku ya Yoga Kimataifa hubeba dhana inaangaza umuhimu wa Yoga na matokeo yake chanya kwenye jamii, " amesema
Aidha amesema katika maazimio ya mkutano mkuu wa Umoja wa Matifa juu ya Siku ya Kimataifa ya Yoga ulitambulisha kwamba Yoga inatoa mbinu kamili na kusambaza taarifa kuhusu manufaa ya kufanya mazoezi ya Yoga kwa afya ya watu duniani.
Waongozaji wa mchezo wa Yoga wakiongoza washiriki walioshiriki katika Siku ya Yoga kimataifa iliyofanyika jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Said Yakub (katikati) akishiriki kufanya mazoezi ya Yoga .Kushoto ni Balozi wa India nchini Tanzania Binaya Pradhan


.jpeg)






.jpeg)

Matukio mbalimbali katika picha wakati wa maadhimisho ya Siku ya Yoga Kimataifa yaliyofanyika jijini Dar es Salaam
Home
HABARI
WATU 1000 DAR, WENGINE MIKOA TISA WASHIRIKI SIKU YA KIMATAIFA YA YOGA, WIZARA YATOA UJUMBE KWA WATANZANIA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...