Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt Ashatu Kijaji (Mb.) ameipongeza Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO ) kwa ubunifu wa utengenezaji wa mitambo mbalimbali kwa gharama nafuu pamoja na vifaa tiba vinavyookoa fedha nyingi kwa kuagiza vifaa hivyo nje ya nchi.


Waziri Kijaji ameyasema hayo alipotembelea Taasisi hiyo Juni 3, 2023 kuona maendeleo ya Mtambo wa Kuchakata Sukari ambao utakuwa na uwezo wa kuchakata Tani 200 za miwa ambazo zitakuwa Sawa na wastani wa Tani 10 za Sukari pamoja na mitambo mingine inayozalishwa na TEMDO

Aidha, Dkt. Kijaji ameishauri Taasisi hiyo kuendelea kutangaza na kuelimisha umma kuhusu bidhaa inazozitengeneza hususani mitambo hiyo pamoja na vifaa tiba kwa ajili ya Hospitali na Zahanati ambavyo vinasaidia Serikali kupunguza gharama ya kuagiza vifaa hivyo nje ya nchi.

Akitoa maelezo kwa Waziri, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. amesema TEMDO imebuni na kutengeneza vifaa tiba vya hospitali na zahanati nchini ikiwemo Vitanda vya Kujifungulia mama wajawazito, Vitanda vya Kulazia Wagonjwa, Makabati ya kuhifadhia vitu vya Wagonjwa, Majokofu ya kuifadhia Maiti, Kiteketezi cha Taka hatarishi zinazo zalishwa na mahosipitali na n.k.

Aidha Prof. Kahimba amesema mitambo mingine inayotengenezwa na TEMDO ni pamoja na mtambo wa kukamulia mafuta ya alizeti, mitambo ya bei nafuu ya kuchuja na kusafisha mafuta ya alizeti (sunflower oil mini-refinery plants), mtambo mdogo wa kuchakata sukari, mtambo wa kusindika zabibu pamoja na mtambo wa kuzalisha umeme wa upepo na jua kwa kutumia teknolojia rahisi na kwa gharama nafuu.

Aidha, Prof Kahimba pia alieleza kuwa TEMDO imefanikiwa kutengeneza Mtambo wakuchakata zao la muhogo wenye uwezo wa kuchakata Tani 10 za muhogo ambazo ni sawa na wastani wa Tani 3 za unga wa Muhogo, Mtambo huo una uwezo wa kuchakata muhogo kutoka shambani na kuwa unga tayari kwa mlaji siku hiyo hiyo na mtambo wa kuchakata zao la mhogo.























Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...