Waziri wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Angellah Kairuki akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha waganga wakuu na waratibu wa Ukimwi wa halmashauri kilichofanyika leo 12juni 2023 katika ukumbi wa Mountmeru mkoani ARUSHA
Na.VERO IGNATUS,ARUSHA
SERIKALI imesema imeendelea kusimamia huduma za ustawi wa jamii katika eneo la familia,malezi makuzi maendeleo ya awali ya mtoto,huduma kwa wazee,na watu wenye ulemavu,ambapo hadi kufikia Februari, 2023, jumla ya Watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi 335,971 walitambuliwa kati ya hao 26,000 sawa na 7.7% walipewa huduma mbalimbali kama Chakula, Malazi, mavazi na matibabu, mashauri 13,926 ya ukatili wa kijinsia yaliripotiwa kati ya hayo 7,142 sawa na 56% yalikuwa ni mashauri dhidi ya Wanawake na 6,784 sawa na 51% yalikuwa ukatili dhidi ya Watoto,ambapo mashauri 1,199 yalifikishwa Mahakamani kati ya hayo 430 sawa na 36% yalitolewa hukumu.
Hayo yamesemwa na Waziri wanchi ,Ofisi ya Rais TAMISEMI,Mhe,Angellah Kairuki wakati akifungua kikao kazi cha waganga wakuu na waratibu wa ukimwi wa halmashauri kilichofanyika leo Juni 12 katika hoteli ya mountmeru ,kilichoambatana na uzinduzi wa mfumo wa kieletroniki wa usimamizi wa taarifa za mfumo wa (PVMIS) amewasisitiza Waganga wakuu wa halmashauri kuhuisha kamati za Ulinzi kwa wanawake na watoto katika ngazi zote, Kuhakikisha mashauri ya kesi za Watoto, Ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto unasimamiwa ipasavyo mahakamani,kuendelea kuwatambua watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi na kuwanganisha na huduma stahiki.
Aidha mhe,Kairuki amesema kuwa Takwimu za Utafiti wa Hali ya Afya, Demografia na Viashiria vya Malaria uliofanyika mwaka, 2022 unaonyesha kuwa tatizo la Lishe duni nchini limeendelea kupungua,Takwimu hizo zinaonesha kuwa kiwango cha tatizo la udumavu miongoni mwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano kimepungua kutoka 34% mwaka 2015 hadi 30% mwaka, 2022; uzito pungufu umepungua kutoka 14% mwaka, 2015 hadi 12% mwaka, 2022 na ukondefu umepungua kutoka 5% mw Jukumu kubwa la Ofisi ya Rais TAMISEMI ni kuendelea kusimamia Afua za Lishe ikiwa ni pamoja na kupeleka huduma za lishe katika ngazi ya wananchi.
‘’Ili kuweza kufikia dhima hii sisi viongozi ngazi ya Mikoa na Halmashauri tunao wajibu wa kuhakikisha kuwa mambo yafuatayo yanatekelezwa ipasavyo na kwa haraka zaidi, Waganga Wakuu wa Wilaya wasimamie utekelezaji wa afua za lishe katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya, Waganga Wakuu wa Halmashauri mnatakiwa kuhakiki taarifa kabla ya kutumwa sehemu husika ili kuweza kutambua viwango sahihi vilivyofikiwa katika utekelezaji wa Mkataba wa Lishe,utekelezaji wa Afua ya siku za Afya na Lishe inayotekelezwa katika vijiji na mitaa uimarishwe na pia ujumuishe utoaji wa huduma za mkoba, kwani afua hiyo imeonekana kuwa na tija katika kufikisha huduma za afya na lishe karibu na wananchi, Halmashauri ziendelee kutenga shilingi 1,000 kwa kila mtoto mwenye umri chini ya miaka mitano katika maeneo yao na kuhakikisha kuwa usimamizi unafanyika ili zitumike kutekeleza afua za lishe zenye kuleta matokeo chanya na ya haraka’’alisema Kairuki
Nimetaarifiwa kwamba Mfumo huu (*M-mama*) umeanza katika Mikoa 14 na unatarajiwa kuenea nchi nzima Kabla au ifikapo mwezi Oktoba 2023 ukiwa na lengo la kupunguza Vifo vya akinamama na Watoto Wachanga Vitokanavyo na uzazi. Mfumo huu unalenga kutatua changamoto kuu tatu ambazo ni: Ucheleweshaji wa maamuzi katika ngazi ya kaya, uchelewaji kufika katika kituo cha kutolea huduma na Uchelewaji katika kupata huduma Stahiki katika Vituo vyetu vya kutolea hudumaza afya.
Matokeo ya Awali katika Mikoa ya Shinyanga inaonesha kwamba kupitia mfumo huu Vifo vya akinamama vimepungua kwa asilimia 38 na kwa Watoto Wachanga kwa asilimia 45.Hivyo Ninaomba kutoa rai yangu kwenu kuhakikishamfumo huu unatumika ipasavyo ili tuweze kuokoa Maisha ya akinamama Wetu na Watoto Wetu wenye uhitaji wa huduma za dharura na kuunga Mkono jitihada za Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mhe.Kairuki amewataka jambo hilo Kwenda sambamba na swala la kuhakikisha wanasimamia vyema utekelezaji wa maswala ya Lishe mpaka ngazi ya jamii kwa kuhakikisha Mikataba iliyosainiwa baina ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wakuu wa Mikoa na kushuka mpaka ngazi ya jamii inatekelezwa ipasavyo,pamoja na kuhakikisha wanasimamia ipasavyo Masuala ya siku ya Afya ya Lishe na Kijiji kwa kuadhimisha siku hizo katika vijiji vyote 12,318 nchini kote,pia wahakikishe kwamba Fedha ambazo zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza afua za lishe zinasimamiwa na kufanya shughuli kusudiwa na hivyo viashiria vyote 14 kutekelezwa kwa asilimia 100.
Aidha, nichukue nafasi hii kuwaelekeza Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kuwa kafanyeni ukaguzi wa bidhaa za afya kwa ushirikiano kati ya Idara ya Afya na Wakuu wa Idara nyingine ikiwa ni pamoja na wakaguzi wa ndani, Vifaa tiba, mashine za maabara na X-ray zilizosambazwa katika Vituo vya kutolea huduma za afya, Wahandisi wa vifaa tiba ngazi ya Halmashauri na watumiaji wa vifaa wanajengewe uwezo ili waweze kumudu kuvitumia na kuvifanyia ukarabati au matengenezo Kinga.
Aidha amesisitiza kuwa taarifa zote za huduma za VVU/UKIMWI zilizotolewa kwa wananchi zikusanywe, zihakikiwe na ziingizwe katika mifumo ya kutolea huduma za afya ya Serikali iliyohakikiwa na kusimikwa katika vituo vyetu vya kutolea huduma za afya kwa wakati,fedha zote za programu, zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa, kulingana na mpango kazi wa programu husika kama ulivyoidhinishwa na Global fund hakikisheni kuwa taarifa zote zinazohitajika kwa mujibu wa mwongozo wa Global Fund zitumwe kwa wakati, na mikataba ya utendaji kazi iandaliwe na kusainiwa kati ya OR-TAMISEMI na Waganga Wakuu wa Mikoa kuhusu suala hili.
Akizungumza katika uzinduzi wa mfumo wa kieletronikiwa usimamizi wa taarifa za mfumo wa mshitiri (PVMIS)mkurugenzi wa huduma za afya,ustawi wa jamii na lishe katika ofisi ya Rais TAMISEMI,Dkt.Ntuli Kapologwe ameipongeza serikali ya uswisi kwa kufadhili uundwajii wa mfumo huo kupitia mradi wa HPSS Tuimarishe Afya.
Sambamba na hayo SERIKALI imesema kuwa mwaka 2022/2023 idadi ya Ajira imeongezeka zaidi na kufikia Watumishi 8,070,japo kuwa idadi hiyo haijaweza tatua kabisa changamoto ya uchache wa watumishi wa afya,ambapo imesema ahadi yake ni kuendelea kuajiri na kuziba pengo katika maeneo yenye upungufu mkubwa kama Wataalam wa Macho, Meno na Mionzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...