NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
SEKTA ya Elimu hasa Shule za Kitanzania zimeshauriwa kutengeneza mashirikiano na vyuo kutoka Mataifa mbalimbali ili kuweza kutoa wasomi wengi ambao wataweza kukubalika kwenye mataifa mengine.
Ushauri huo umetolewa hapo jana Julai 29,2023 Mwalimu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Emmanuel Mjema katika Mahafali ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Ahmes Bagamoyo mkoani Pwani.
Amesema ili kuweza kutoa wasomi ambao wataweza kukubalika ulimwenguni, kuna umuhimu mkubwa shule zetu ziwe na mashirikiano na vyuo vya nje ili watakapomaliza waweze kufanya kazi kokote ulimwenguni.
"Tunapotoa elimu tuangalie kwamba Kimataifa iko vipi, wenzetu wapo katika viwango gani ili kuongeza ufanisi mkubwa kwenye suala la elimu nchini". Amesema Prof. Mjema.
Pamoja na hayo Prof.Mjema ameipongeza shule ya Sekondari Ahmes kwa kuweza kufanya vizuri kwenye matokeo ya kidato cha Sita kwa miaka miwili mfululizo ambapo kwa matokeo ya sasa wameweza kushika nafasi ya kwanza kitaifa.
Nae Meneja wa Shule ya Ahmes, Bw. Sam Mjema amesema mabadiliko ya walimu kwenye vituo vyao vya kazi (uhamisho wa mara kwa mara) unachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza ufaulu kwa wanafunzi kwa maana walimu wanakosa muda wa kujifunza kupitia makosa.
Aidha amesema kuwa ushirikiano katia ya walimu na wanafunzi kwa kiasi kikubwa imechangia shule hiyo kuendelea kufanya vizuri kuanzia ngazi ya Mkoa hadi Kitaifa.
Kwa Upande wa Mwanafunzi ambaye amefanya vizuri kwenye matokeo hayo Derick Machibya amesema uhusiano mzuri na walimu kwenye masomo mbalimbali pamoja na wanafunzi wenzake umekuwa chachu ya kufanya vizuri kwenye masomo yake.
Mwalimu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Emmanuel Mjema akikabidhi vyeti kwa Wahitimu wa Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Ahmes kwenye Mahafali ambayo yamefanyika Jana Julai 30,2023 Bagamoyo mkoani Pwani.
Mwalimu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Emmanuel Mjema akizungumza kwenye Mahafali ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Ahmes ambayo yamefanyika Jana Julai 30,2023 Bagamoyo mkoani Pwani.
Meneja wa Shule ya Ahmes, Bw. Sam Mjema akizungumza kwenye Mahafali ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Ahmes ambayo yamefanyika Jana Julai 30,2023 Bagamoyo mkoani Pwani.
Wahitimu wa Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Ahmes wakiwa kwenye Mahafali ambayo yamefanyika hapo Jana Julai 29,2023 Bagamoyo mkoani Pwani.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...